January 25, 2025

MBUNGE MAVUNDE AWAWEZESHA KIUCHUMI WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SABASABA JIJINI DODOMA











Na Mwandishi wetu,odoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mh. Anthony Mavunde ameahidi kuwaendeleza kiuchumi wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Jijini Dodoma kwa kuwapatia miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kuongeza kipato chao.

Mh. Mavunde kayasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Kikundi cha Twiga cha wafanyabiashara wadogo wadogo uliofanyika ndani ya Soko la Sabasaba.

“Tunaishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S . Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu yanayoendelea ndani ya Jiji la Dodoma.

Nipo hapa leo kama Mwanachama mwenzenu wa kikundi cha Twiga ambacho tulikiasisi pamoja.

Nina furaha kubwa kusikia mipango iliyopo ya kuongeza miradi ya kujiimarisha kiuchumi,nitajitahidi kuendelea kuwashika mkono ili muweze kusimama kiuchumi.

Pamoja na mradi wa Shamba la mbogamboga nililowapatia,nitawaongezea na mradi wa kutoa huduma ya maji safi kwa wafanyabiashara wa soko la Sabasaba,TV ya inchi 55 kww ajili ya mradi wa kuonesha mpira na Shilingi Milioni 5 kutunisha mfuko wa Kikundi“Alisema Mavunde


Akitoa shukrani kwa niaba Mlezi wa Kikundi cha Twiga *Mama Anna Nyigana* amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwajali na kuwaendeleza kiuchumi wafanyabiashara hao wadogo na kuahidi kusimamia ipasavyo miradi hiyo ili iweze kuleta tija ya kiuchumi kwa wanakikundi.

No comments:

Post a Comment