Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akitoa amri ya kukamatwa kwa viongozi wa AMCOS ya Namapwia kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za AMCOS hiyo.
Baadhi viongozi wa AMCOS ya Namapwia waliokamatwa
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Nachingwea iliyokabidhiwa viongozi wa AMCOS ya Namapwia kwa ajili ya uchaguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa mali za AMCOS hiyo.
Na Fredy Mgunda, Nachingwea Lindi.
Viongozi wa AMCOS ya Namapwia wamekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kufuatia uchunguzi uliofanywa kuhusu ubadhilifu wa fedha za wakulima na upotevu wa mazao.
Uchunguzi huo ulifanywa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanachama wa chama hicho, na ripoti ya ukaguzi kubaini kwamba viongozi hao walihusika katika ufisadi wa mazao na malipo yasiyostahili kwa wakulima.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo alitoa agizo la kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya wahusika na kusema kuwa wote watapelekwa polisi kwa mahojiano zaidi.
Agizo hilo lilitolewa wakati wa ziara yake kata ya Namapwia ambapo alikabidhiwa ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na timu ya ukaguzi iliyoongozwa na Afisa Ushirika Wilaya ya Ruangwa, Patrobas.
Ripoti ya ukaguzi iliyofanywa kati ya tarehe 15 hadi 22 Oktoba 2024 ilibaini upotevu wa tani 21 za mazao, pamoja na ulipaji wa fedha kwa wakulima ambao hawajauza mazao yao kupitia AMCOS hiyo.
Vilevile, ilibainika malipo ya zaidi ya milioni tatu msimu wa ufuta ambazo hazikuingizwa kwenye akaunti rasmi ya AMCOS, huku baadhi ya malipo hayo hayakuwa yameidhinishwa na kamati ya chama hicho,upotevu wa fedha shilingi milioni 60 ambazo walizilipa kwa kugawana wajumbe wote.
Kiongozi wa timu ya ukaguzi, Patrobas, alieleza kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho walitengeneza wakulima feki na kufanya malipo ya fedha za mazao ambayo hayakuuzwa.
Patrobas aliongeza kuwa mfumo wa biashara wa chama hicho ulikuwa na dosari, hali iliyosababisha upotevu mkubwa wa fedha.
Kwa upande wake Mrajisi wa Vyama Ushirika Mkoa wa Lindi, Keneth Shemdoe, aliifuta bodi ya AMCOS ya Namapwia na kuunda kamati ya mpito ili kuendeleza shughuli za chama hicho.
Shemdoe pia alitoa agizo la kuwaajiri meneja wenye kiwango cha elimu cha stashahada au shahada ili kuendana na mahitaji ya sasa, huku akisisitiza chama hicho kuandaa akaunti rasmi ikiwa na orodha ya hisa za wanachama pamoja na daftari la taarifa zao ndani ya muda wa mwezi mmoja.
Diwani wa kata ya Namapwia, Mheshimiwa Omari Muhamed Lingumbende, amepongeza kwa hatua zilichukuliwa kwa kukamatwa viongozi ha
No comments:
Post a Comment