Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kongamano la Kimatifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha, Desemba 6, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kongamano la Kimatifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha, Desemba 6, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza Samson Ibrahim wa Kampuni ya Dahua Technology (kulia) wakati alipotembelea banda la maonesho la kampuni hiyo kabla ya kuzungumza katika Kongamano la Kimatifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, Desemba 6, 2024. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa awataka wahandisi wote nchini wazingatie miiko na maadili ya taalum hiyo ikiwemo kuitekeleza miradi ya ujenzi kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha halisi iliyotolewa.
“Sote tunatambua kwamba wapo wachache katika taaluma yenu ya uhandisi ambao wanaichafua kwa kufanya matendo ambayo ni kinyume na taaluma lakini pia ni kinyume na maadili.”
“Matendo hayo ni pamoja na rushwa, ubadhilifu, na ukosefu wa weledi. Hii si tu kwamba inachafua taaluma ya uhandisi, bali pia inaharibu taswira ya nchi”.
Ameyasena hayo leo (Desemba 06, 2024) kwenye Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Bodi ya usajili wa Wahandisi isimamie maadili ya kihandisi na makampuni ya kihandisi kwa mujibu wa sheria ili kulinda hadhi ya uhandisi nchini.
Waziri Mkuu ametoa rai kwa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) kuendelea kushirikiana na vyombo mbalimbali kuwabaini wanaokiuka maadili na sheria na kuchukua hatua stahiki kwani taaluma ya uhandisi ni muhimu na inapaswa kutunza na kulinda heshima yake.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mita na Usalama Barabarani kuhakikisha kuwa vizuizi na vituo vya ukaguzi vinazingatia usalama wa watumiaji na tahadhari zote za kiusalama.
“Wahandisi na wataalamu wetu mnao wajibu wa kuendelea kubuni na kupendekeza mifumo bora ya alama za barabarani, usimamizi wa miundombinu ya barabarana uwekaji wa vituo vya ukaguzi ili kupunguza ajali na madhara yake.”
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Serikali imeendelea kufanya maboresho ya kanuni ili kusaidia wakandarasi na wahandisi wazawa washiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali hapa nchini.
“Kwasasa thamani ya miradi ambayo haizidi shilingi bilioni 50 inakwenda kwa wazawa na hili kwa kiasi kikubwa imeleta mabadiliko makubwa kwenye Sekta ya Ujenzi, pia tumelegeza masharti ya TANROADS kwenye ununuzi ili kanuni hii iendane na masharti rafiki pamoja na kuimarisha Kitengo cha Usimamizi wa Miradi cha TECU kilichopo TANROADS ambapo wameendelea kusimamia miradi kwa viwango na ubora badala ya kutegemea utegemezi wa makampuni ya nje.”
Naye, Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) Mhandisi Dkt. Gemma Modu ameipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuongeza ushiriki wa wazawa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo kwa kiasi kikubwa inafungua fursa kwa wahandisi wazawa na mafundi wote nchini.
“Kutokana na kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, tutaendelea kushirikiana na Serikali na tunaahidi kuendeleza na kukuza kiwango cha ujuzi na kusisitiza uzalendo na uadilifu katika utekelezaji wa miradi.”
No comments:
Post a Comment