Wananchi wa kijiji cha
CHEKERELI Kata ya Mabilioni Wilayani
Sam,Mkoani Kilimanjaro, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa
maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 30 ambapo kutokana na ukosefu huu, wamekuwa
wakilazimika kutumia maji ya Mto Ruvu kwa mahitaji yao ya kila siku, hali
ambayo imechangia ongezeko la magonjwa ya tumbo na mengine yanayosababishwa na
matumizi ya maji machafu.
Wananchi kijiji cha Chekereli
LENI KIVUNGE na SILVANO HUSSEIN
Wakizungumza kijijini hapo walieleza changamoto wanazokabiliana nazo.
"Tunatembea umbali wa kilomita tano kila
siku kufuata maji ya mto tunalazimika kutumia maji haya kwa kunywa, kupika, na
shughuli nyingine licha ya kujua yanaweza kuwa na madhara kwa afya zetu,"
alisema Leni
Wananchi hao wameeleza kuwa
hali hiyo imekuwa ikisababisha mzigo mkubwa, hususan kwa wanawake na watoto
ambao ndio hufanya kazi ya kuchota maji.
Aidha, wameeleza kuwa hali
hiyo imeathiri maendeleo yao kwani muda mwingi hutumika kutafuta maji badala ya
kushiriki shughuli za kiuchumi.
Akizungumzia kadhia hiyo
Silvano amesema wao wamekuwa wakitumia maji hayo ambayo sia safi wala salama
ambayo yamekuwa yakibeba takataka nyingi ambazo ni hatari kwa Maisha yao.
“Kwa hiyo tunaomba mbunge
atusaidie sana ikiwezekana atutembelee kijijini kwetu aone na tumpe mawazo yetu
ili aweze kutusidia tuondokane na changamoto hii’Alisema Silvano
Mbunge wa Same Magharibi
almaarufu “mwana wa Kaya”akiwa katika ziara ya kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka
2020-2025 aliyoipa jina la Operesheni Ahadi, amesikia kilio hicho na kutoa
msaada wa mabomba 25 kwa ajili ya kusambaza kijijini hapo ili kuwasaidia
kupunguza umbali wa kufuata maji.
"Sasa Chekereli
ninawapatia roller za maji 25 kwa ajili
ya kusambazia maji wananchi wangu wapate maji kule kwa sababu nao wamenipa
kura mimi mbunge ili ikifika 2025 wakija
hapa wakisema ntafanya hivi vile watakuta Mathayo keshafanya" alisema
Mathayo.
Mathayo amesema anajua kuwa
wananchi wa eneo hilo walikuwa wakipata shida kubwa ya maji hivyo mradi huo
utakapokamilika utasaidia kusambaza maji katika eneo la Chekereli na wakina
mama itasaidia kuwatua ndoo kichwani ili wasihangaike sana kwa sababu wamezaa
mtoto wa kiume anaitwa Mathayo.
Wananchi wameishukuru mbunge
Mathayo kwa hatua hiyo ya awali, lakini wamesisitiza haja ya kutekelezwa kwa
mradi wa maji safi haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha yao na kuboresha hali
ya maisha.
No comments:
Post a Comment