December 11, 2024

WAKINAMAMA CHALINZE WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA NISHATI SAFI





Maneno haya yamesema na Bi. Lilian Skawa kwa niaba ya wakinamama wa Chalinze mbele ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze na WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Wenye Ulemavu Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati wakipokea  majiko ya gesi 118 kwa mama lishe wa kata 15 za Jimbo la Chalinze. 

Ndg. Ridhiwani  Kikwete amesema lengo kubwa la kugawa majiko haya ya gesi ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika  kutunza mazingira na kuwafanya wananchi kuondokana na matumizi ya nishati chafu.

" Sasa mtakwenda kupika chakula kwa haraka na kwa Usafi na hii itasaidia katika shughuli zenu kwa pamoja tutamuunga Mhe. Rais  kwenye uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambayo italinda afya zenu pia" amesema

Afisa Maendeleo ya Jamii na mratibu wa dawati la Jinsia wa Halmashauri hiyo Recho Mnguruta amesema  majiko hayo yatakwenda kuwasaidia Wanawake wajasiriamali hao kuondokana na  kutumia kuni na mkaa.

Naye Bi. Lilian Skawa mkazi wa Msata amemshukuru Mbunge huyo wa Jimbo hilo kwa kuwapatia majiko hayo ambayo yatawarahisishia kwenye kazi yao kupika kwa haraka na kuwapatia wateja wao chakula cha moto muda wote.

Amesema kipindi cha mvua walikuwa wanakabiliana na changamoto ya mkaa ambao wanapata kwa shida na ukiwa umelowa hivyo kwasasa wanakwenda kuwa na mabadiliko ya kupika kwa wakati chakula na kwa Hali ya Usafi.

No comments:

Post a Comment