Timu ya Bunge ya Mpira wa Wavu Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo kati yao na Timu ya Bunge ya Sudan ya Kusini kushindwa kufanyika kutokana na timu hiyo kutofika uwanjani. Timu za Bunge la Tanzania zipo Mombasa Nchini Kenya kushiriki michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mchezaji wa Timu ya Riadha kutoka Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Anatropia Theonist akishiriki katika mbio za mita 1500 katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya. Mheshimiwa Anatropia alishika nafasi ya kwanza katika mbio hizo na mbio za mita 400.
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Kamba Wanaume wakivuta kamba dhidi ya wapinzani wao Timu ya Kenya katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya.Timu ya Bunge la Tanzania iliibuka kidedea katika mchezo huo.Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Kamba Wanawake wakivuta kamba dhidi ya wapinzani wao Timu ya Kenya katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya.Timu ya Bunge la Tanzania iliibuka kidedea katika mchezo huo
Mheshimiwa Anatropia ameshika namba moja katika mbio za mita 1500 akiwashinda wapinzani kutoka Bunge la Uganda,Kenya, Rwanda na Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Vilevile katika mbio za mita 400, aliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza akimpita mpinzani wake wa karibu kutoka Bunge la Uganda.
Aidha, katika mbio za mita 100 Mheshimiwa Condesta Sichwale alishika nafasi ya tatu huku Mheshimiwa Saada Mansour Hussein akishika nafasi ya tano katika mbio hizo.
Katika mbio za wanaume mita 100 Mheshimiwa Jaffar Chege aliibuka mshindi wa tatu nyuma ya wapinzani wake kutoka Bunge la Kenya na Uganda.
Kwa upande wa mbio za kupokezana vijiti, Timu ya Tanzania ya Riadha wanawake iliibuka mshindi wa pili huku riadha wanaume wakiibuka mshindi wa nne.
Kwenye mchezo wa Kamba, Timu ya Tanzania Wanaume ilijizolea pointi 2-0 baada ya kuiburuza timu ya Wanaume ya Bunge la Kenya.
Kwa upande wa Timu ya Wanawake ya Kamba Bunge la Tanzania wameibuka kidedea kwa pointi 2-0 baada ya kuigaragaza Timu ya Wanawake ya Bunge la Kenya.
Nayo timu ya Wanawake ya Mpira wa Wavu ya Bunge la Tanzania imejinyakulia pointi za mezani baada timu pinzani ya Bunge la Sudani Kusini kushindwa kufika uwanjani.
No comments:
Post a Comment