December 08, 2024

NAIBU WAZIRI MKUU DKT DOTO BITEKO ASHIRIKI MBIO ZA UDSM MARATHON 2024 KAMPSI YA MLIMANI LEO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko akishiriki mbio za UDSM Marathon 2024 za Chuo Kikuu cha Dar es salaam zilizofanyika mapema asubuhi leo katika Kampasi ya Mlimani jijini Dar es salaamm leo  Jumamosi Disemba 7, 2024. Katika mbio hizo Mhe Biteko ameshiriki fun run ya Kilomita 5 akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salama Kikwete ambaye ni mbunge wa Mchinga pamoja na uongozi wote wa chuo kikuu  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho kikongwe Balozi Mwanaidi Maajar. Lengo la mbio hizo ni kuchangisha pesa ili kujenga kituo cha wanafunzi chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salama Kikwete ambaye ni mbunge wa Mchinga pamoja na uongozi wote wa chuo kikuu  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho kikongwe Balozi Mwanaidi Maajar wakifurahia kuhitimisha salama na kwa mafanikio makubwa mbio za UDSM Marathon 2024 za Chuo Kikuu cha Dar es salaam zilizofanyika mapema asubuhi leo katika Lengo la mbio hizo ni kuchangisha pesa ili kujenga kituo cha wanafunzi chuoni hapo. ya Mlimani jijini Dar es salaamm leo  Jumamosi Disemba 7, 2024. Lengo la mbio hizo ni kujenga kituo cha wanafunzi chuoni hapo.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko  akiongea jambo na  na Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kishiriki mbio za UDSM Marathon 2024 za Chuo Kikuu cha Dar es salaam zilizofanyika mapema asubuhi leo katika Kampasi ya Mlimani jijini Dar es salaamm leo  Jumamosi Disemba 7, 2024. Lengo la mbio hizo ni kuchangisha pesa ili kujenga kituo cha wanafunzi chuoni hapo.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imetumia Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) kushiriki katika mbio za Marathon zilizoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mbio hizo zilizoongozwa na Mhe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa Mchinga pamoja na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) ambayo kilele chake ni Desemba 7,2024. Maadhimisho ya mwaka huu pia inatimia miaka 80 tangu siku hii ilipoanza kuadhimishwa mnamo Desemba 7 mwaka 1944.

Watumishi wa TCAA licha ya kufanya kazi zao za ki udhibiti na kuongoza ndege pia hushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni hatua ya kuweka afya katika hali bora wakati wote.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameongoza mbio za UDSM Marathon za Chuo Kikuu cha Dar es salaam akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa Mchinga pamoja na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam








Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wakiwa kwenye Matembezi na Mbio zilijulikanazo kama UDSM Marathon











Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA wakiwa kwenye picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment