December 20, 2024

MBUNGE WA SAME MAGHARIBI ATOA MCHANGO WA BILIONI MOJA KUBORESHA MAENDELEO






Mbunge wa Same Magharibi, Dkt. David Mathayo, ameonyesha mfano wa uongozi wa vitendo kwa kutoa mchango wa zaidi ya shilingi bilioni moja ili kusaidia maendeleo katika jimbo lake. 

Fedha hizo pamoja na vifaa vingine, vimeelekezwa katika sekta muhimu kama elimu, afya, maji, na uchumi. 

Hali ya furaha imejawa katika jimbo la Same Magharibi baada ya Mbunge wao, Dkt. David Mathayo, kutoa mchango mkubwa wa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi. 

Mchango huo unajumuisha fedha taslimu, saruji, mabati, na vifaa vingine vya ujenzi, ambavyo vimeelekezwa kwa taasisi za serikali na zile za dini.

“Mbunge wetu ametoa mchango mkubwa ambao umeleta tumaini jipya kwa wananchi. Vifaa hivi vitasaidia kuboresha huduma za afya na elimu, na pia kuimarisha miundombinu ya maji katika maeneo mbalimbali ya jimbo.”

Katika ziara yake ya kutembelea kata 20 za jimbo la Same Magharibi, Dkt. Mathayo amekuwa akitimiza ahadi zake kwa vitendo. 

Mchango huu ni sehemu ya jitihada zake za kutatua changamoto zinazowakumba wananchi wa jimbo hilo, kama alivyoeleza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo.
 
“Ni jukumu langu kama kiongozi kuhakikisha wananchi wa Same wanapata huduma bora. Leo tumetoa vifaa hivi ili kuboresha shule, zahanati, na pia miradi ya maji ambayo ni muhimu kwa ustawi wa jamii.”

Mmoja wa wananchi alitoa maoni yake:
“Mchango huu wa mbunge ni wa kihistoria. Tunaona sasa kazi inafanyika, na tunashukuru sana kwa juhudi zake.”

Mchango huu wa Dkt. Mathayo unatoa ishara ya ushirikiano mzuri kati ya viongozi na wananchi katika kusukuma gurudumu la maendeleo. Wananchi wa Same Magharibi sasa wana matumaini makubwa ya maisha bora kupitia juhudi hizi za kimaendeleo.

Hakika ni hatua muhimu kwa maendeleo ya jimbo la Same Magharibi.

No comments:

Post a Comment