December 01, 2024

MADALE WADAU GROUP WATIMIZA MIAKA 10, WAJENGA KITUO CHA POLISI

Umoja wa Madale Wadau Group umefanikiwa kujenga kituo cha polisi kilichogharimu zaidi ya shilingi milioni 250. Mwenyekiti wa kikundi hicho, Stephen Kazimoto, alitoa taarifa hiyo leo, Novemba 30, 2024, wakati wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho. Sherehe hizo zilifanyika katika ufukwe wa Silver Sands, Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Kazimoto alisema kuwa kituo hicho kimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya uhalifu katika maeneo ya Madale. “Tumejenga kituo cha polisi ambacho sasa kinafanya kazi vizuri sana na kimeimarisha usalama ndani ya jamii,” alisema.

Pamoja na hilo, Kazimoto alieleza kuwa kikundi hicho kimeanzisha SACCOS yenye malengo ya kusaidiana wanapokumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo misiba. Aliongeza kuwa SACCOS hiyo inatoa mikopo yenye riba nafuu kwa wanachama, hatua ambayo imewasaidia kuboresha hali zao za kiuchumi na kuchangia pato la taifa.

“Kwa sasa, tumeanzisha mfumo mpya wa kuchangishana na kuweka fedha benki. Tunapokuwa na akiba benki, matatizo ya wanachama yanatatuliwa kwa haraka,” aliongeza.

Mdau Moses Denis amesema umoja huo umelenga kusaidiana kwenye shida na raha na ndiyo jukumu kubwa linalofamywa na umoja huo ambao umekuwa msaada mkubwa kwa wanachama wake. 

Naye Juliana Mugoa anasema kundi LA wadau hao limesaidia kwa kiasi kikubwa wanachama wake hasa inapotokea misiba kwani jambo hilo hutokea ghafla hakuna anajua siku hivyo kutaka wadau kudumu siku zote.

No comments:

Post a Comment