Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini IGP Camillus M. Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Amemhamisha
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ramadhani Ng’anzi kutoka Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabaarani Tanzania kwenda Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma
kuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Maadili ya Jamii.
Nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mkonda
ambaye alikuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam.
Pia
amemhamisha aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniphace Mbao kutoka Dodoma kwenda kuwa Mkuu wa
Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam.
Aidha,
aliyekuwa Mkuu wa Elimu kwa Umma Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania,
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Michael Deleli amemhamishia Makao Makuu ya
Polisi Dodoma kuwa Kaimu Mkuu wa Maadhimisho ya Kitaifa.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassoro Sisiwaya aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania amemhamishia Mkoa wa Kilimanjaro kwenda kuwa
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment