Chama cha Umoja wa madereva pikipiki (Bodaboda) Mbeya Jiji, kimemtaka Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kuhakikisha anagombea tena nafasi hiyo ya Ubunge katika Uchaguzi mkuu ujao 2025 kwakuwa wameridhishwa na utendaji kazi wake hivyo hawatarajii kuwa na mbadala wake.
Akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa madereva hao Kanda ya Sae uliofanyika Disemba 20, 2024 katika Ukumbi wa Mfikemo, Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndg. Aliko Fwanda amesema kuwa umefika wakati wa Wananchi wa Mbeya mjini kuchagua Kiongozi kwa kigezo cha utendaji kazi na sio kwa kutumia mihemko ya Vyama vya siasa.
“Kazi anazozifanya Dkt. Tulia zinaonekana na hatuwezi kuongea uongo, mimi sijahama CHADEMA lakini namuunga mkono hadi keshokutwa. Mimi sina mambo ya konakona na mwakani kwenye Ubunge lazima ugombee na sisi tutakupigia kura wewe sasa nione mtu mwenye karoho ka korosho” Amesisitiza Ndg. Aliko Fwanda
No comments:
Post a Comment