Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia – Tanzania, Bw. Nathan Belete, wakibadilishana Hati ya Mikataba Miwili (2) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 104 (sawa na takribani sh. bilioni 248) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”, katika hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Hafla ya utiaji saini wa
mikataba hiyo imefanyika jijini Dar es Salam kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkazi wa Benki
ya Dunia, Bw. Nathan Belete.
Akifafanua kuhusu mikataba
hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa mkataba wa dola za Marekani milioni 4,
sawa na zaidi ya shilingi bilioni 9.5 ni msaada na Mkataba wa dola za Marekani
milioni 100, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 238 ni mkopo wenye masharti
nafuu.
Alisema mradi wa PAMOJA
uliosainiwa utasaidia kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi kwa wanawake
pamoja na huduma za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia Tanzania Bara
na Zanzibar.
‘’Hili litatimizwa kupitia uimarishaji vikundi vya wanawake kwa kuwajengea ujuzi wa biashara na kuwaunganisha na fursa za masoko, kuongeza fursa za mikopo nafuu kwa vikundi vya wanawake, kuwaongezea upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia mifumo rasmi ya kifedha pamoja na kuimarisha huduma za kukabiliana na ukatili wa kijinsia”, alifafanua Mhe. Dkt. Nchemba,
Alisema mradi huo
utawanufaisha moja kwa moja wanawake wapatao 319,850 na walengwa wengine
399,000, wakiwemo wanafamilia za wanufaika.
Alisistiza kuwa kukuza usawa
wa kijinsia si suala la wanawake pekee bali ni msingi wa Taifa la kidemokrasia,
lenye haki na linalostawi na kuongeza kuwa kuondoa tofauti za kijinsia
kunaboresha uzalishaji na kuimarisha uhimilivu wa kiuchumi.
“Mradi wa PAMOJA ni sehemu ya
utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Taifa
2021/22 - 2025/26, Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya 2050 na pia ni sehemu ya
ajenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye amelipa
kipaumbele suala la usawa wa kijinsia”, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema utekelezaji wa mradi
huo ni ushahidi wa dhamira ya Serikaliya
kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (hususan Lengo la 5) na
kuonesha nia thabiti ya kufanikisha ukuaji wa uchumi unaowajumuisha wote.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete, alisema kuwa mradi
huo utatatua changamoto za kijinsia za kijamii na kiuchumi kwa kuwawezesha
wanawake kiuchumi na kubainisha mila potofu ili kukabiliana na ukatili wa
kijinsia.
Aliiomba Serikali
kuzikutanisha pamoja Wizara zote za kisekta zinazohusika katika utekelezaji wa
mradi huo kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na
Watoto.
Alisema wanatarajia mradi huo utaanza kutekelezwa mapema na kuona matokeo ya utekelezaji pamoja na faida watakazo zipata walengwa wa mradi huo.
Kwa upande wa Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima
(Mb), alimpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada
mbalimbali anazofanya kuwainua wanawake kiuchumi ikiwemo kuwezesha upatikanaji
wa fedha kwa ajili ya mradi wa PAMOJA.
Alisema katika hatua za awali
za utekelezaji wa mradi huo, Wizara yake imeshazindua Sera ya Taifa ya Jinsia
na Maendeleo ya Wanawake pamoja na Mkakati wake ambao uwezeshaji wanawake
kiuchumi ni miongoni mwa malengo yake.
Alisema mradi huo umekusudia
kujenga nyumba salama 10 kwa ajili ya kuwahifadhi Watoto wanaokumbana na
ukatili wa kijinsia pamoja na kujenga vituo 200 vya malezi salama na makuzi
ambapo vituo 184 vitakuwa Tanzania Bara na 16 vitajengwa Zanziber.
“Afisa Ustawi wa Jamii na
Maendeleo ya Jamii wamekuwa wakihangaika kupata ofisi za kufanyiakazi na kutoa huduma
pamoja na vifaa kazi ikiwemo usafiri, sasa
kwa kutumia fedha hizi watapata Ofisi 40 za maafisa Maendeleo ya Jamii
na Ofisi 40 za Maafisa Ustawi wa Jamii”, alifafanua Mhe. Dkt. Ngwajima.
Alisema fedha hizo zitasaidia
kuwachangamsha wanawake kiuchumi, kupata elimu ya kibiashara, mitaji pamoja na
kufanya biashara wakiwa na uelewa mpana kwa sababu wataalam wamewezeshwa
kuwafikia popote walipo.
Aliahidi kuhakikisha fedha
hizo zitatumika kikamilifu kwenye mradi iliyokusudiwa na kuleta matokeo Chanya.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia – Tanzania, Bw. Nathan Belete, wakionesha Hati ya Mikataba Miwili (2) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 (sawa na takribani sh. bilioni 248) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”, katika hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (katikati) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia – Tanzania, Bw. Nathan Belete, wakisaini Hati ya Mikataba Miwili (2) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 (sawa na takribani sh. bilioni 248) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”, wakishuhudiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima (Mb), katika hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia – Tanzania, Bw. Nathan Belete, (kushoto) na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima (Mb), (katikati)wakiteta jambo baada ya kusaini Hati ya Mikataba Miwili (2) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 (sawa na takribani sh. bilioni 248) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”, wakishuhudiwa na katika hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kulia, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia – Tanzania, Bw. Nathan Belete, wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia, baada ya kusaini Hati za Mikataba miwili (2) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 (sawa na takribani sh. bilioni 248) kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”, katika hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania na Benki
ya Dunia (WB) wamesaini mikataba miwili (2) yenye thamani ya dola za Marekani
milioni 104, sawa na takriban shilingi bilioni 248, kwa ajili ya kusaidia
utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia nchini Tanzania, maarufu kama
“PAMOJA”.*************************
Na Farida Ramadhani na
Chedaiwe Msuya, WF - Dar es Salaam‘’Hili litatimizwa kupitia uimarishaji vikundi vya wanawake kwa kuwajengea ujuzi wa biashara na kuwaunganisha na fursa za masoko, kuongeza fursa za mikopo nafuu kwa vikundi vya wanawake, kuwaongezea upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia mifumo rasmi ya kifedha pamoja na kuimarisha huduma za kukabiliana na ukatili wa kijinsia”, alifafanua Mhe. Dkt. Nchemba,
Alisema wanatarajia mradi huo utaanza kutekelezwa mapema na kuona matokeo ya utekelezaji pamoja na faida watakazo zipata walengwa wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment