November 09, 2024

WATUMISHI WA ARDHI JIJI LA DODOMA WAPEWA SIKU 30 KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI




Na Eleuteri Mangi, WANMM
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe. Degratius Ndjembi ametoa siku 30 kwa watumishi wa Ardhi jiji la Dodoma kutatua migogoro na changamoto za ardhi na kupata majawabu ifikapo Desemba 10 2024.

Waziri Ndejembi amesema hayo Novemba 8, 2024 wakati wa kikao chake na watumishi wa Ardhi Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma pamoja na jiji la Dodoma ambapo amesema mwelekeo wake ni utendaji kazi kwa weledi, kutenda kazi kwa haki na kuwahudumia wananchi kwanza.

Waziri Ndejembi amesema watumishi hao kama watashindwa kutatua changamoto ya ardhi katika jiji hilo atawachukulia hatua kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kupanga jiji la Dodoma vizuri, kutenga maeneo ya bustani za kupumzikia na maeneo  ya michezo ya watoto kwa kuangalia mahitaji ya sasa na baadaye. 

Aidha, amewaagiza watumishi wa serikali ambao ni waajira ya kudumu wafanye kazi ya kuingia kwenye mfumo na kutoa huduma kwa wananchi ambapo amesisitiza kazi hiyo isifanywe wa watumishi wa mkataba na wanaojitolea ili kumaliza changamoto ya kupanga kiwanja kimoja kwa watu wawil. 

Waziri Ndejembi amewataka watumishi ambao hawawezi kuendana na kasi ya Wizara na ukuaji wa Makao Makuu katika jiji la Dodoma waseme ili wahamishiwe sehemu nyengine huku akiweka wazi kuwa asilimia 90 ya watumishi wa jiji la Dodoma hawapokei simu za wanamchi wanaouliza na kuhitaji huduma za ardhi kuhusu maeneo yao na kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu.

Amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga kuwasiliana na vyombo vya dola kuwachukulia hatua watumishi wawili Herman Chizoza na Palangyo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi kwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni sita kwa wateja waliokuwa wanahitaji huduma ya Ardhi katika ofisi hizo. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewata Wakurugenzi wote kusimamia maagizo ya viogozi na kuwasisitiza watumishi hao kuyajua na kutekeleza maagizo yote yanayotoka kwenye mfumo ili sekta ya ardhi itoe huduma stahiki kwa wananchi na kusemwa vizuri.

Naye Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga amesema wameyapokea na watayafanyia kazi maelekezo ya Waziri Ndejembi na kuwasisitiza kupokea simu za wananchi kwa kuwa hao ndiyo waajiri wao, wasipopokea simu wananchi waende wapi kwa kuwa watumishi hao ndiyo wenye majawabu ya mahitaji ya wananchi.

No comments:

Post a Comment