Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wasisahau safari iliyowafikisha katika nchi ya amani na maendeleo.
Dkt. Biteko amesema hayo Novemba 22, 2024 katika wakati akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni za Serikali za Mitaa zilizofanyika katika Kata ya Lulembela, Wilaya ya Mbogwe, Geita.
Amewataka kujitokeza kuwachagua viongozi wenye maono na mwelekeo wa kuwaunganisha kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa. “ Tunachagua viongozi wenye uelewa wa matatizo na kujua namna ya kutatua matatizo ya wananchi” amesema Dkt. Biteko.
Wanambogwe mna haki ya kuchagua kati ya maendeleo na maneno, kwa kuwa watu wangependa kupata maendeleo na wamechoshwa na maneno yanayolenga kuwagawa watu. “Wenzetu wanakuja kusema na kutukana watu” watu wa Mbogwe ikifika tarehe 27 jitokezeni kwenda kupiga kura” Hatuhitaji ushindi wa kubebwa, bali watu waliojiandikisha wajitokeze kupiga kura.
“ Nimekuja kuwaomba mtuunge mkono kwa kupiga kura na kuchukua vijiji na vitongoji vyote” ameomba
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Nicolaus Kasendamila amewashukuru wagombea waliopitishwa na kusema hadi sasa CCM imepitishwa kwa asilimia 84 katika ngazi mbalimbali katika uchaguzi huu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mbogwe amesema wagombea 301 kati ya 335 CCM hawakupata upinzani na wagombea 70 kati ya 87 katika ngazi ya vijiji wamepita bila kupingwa.
Mbunge wa Mbogwe, Mhe. Nicodemas Maganga amewapongeza wanaCCM walioteuliwa kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.
Amewaomba kuondokana na vitendo vyote vya uvunjifu wa maadili ikiwemo vitendo vya rushwa.
Amesema wilaya hiyo inapendeza kwa vile kuna karibu kila kitu, kama kuna mapungufu ni madogo. “ Wagombea mmeaminiwa na watu hivyo mtatakiwa kufanya kazi bila kumruhusu shetani,” amesema.
Hata hivyo, amewataka kushirikiana na wapinzani ili kuleta maendeleo ya watu ambao ndio lengo la CCM.
“ Mgeni rasmi umechangia kuleta maendeleo ya Wilaya ya Mbogwe nasi tunakuomba ukamwambie Mheshimiwa Rais kuwa tuko imara kutafuta maendeleo ya wananchi” amesisitiza.
No comments:
Post a Comment