Wito umetolewa kwa wakazi wa mitaa ya Tanga Mjini kuwachagua wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaogombea nafasi za uenyeviti wa mitaa pamoja na wajumbe wao kwani hao ndiyo wenye dhamira na uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, Novemba 24, 2024, kwa nyakati tofauti alipokuwa akiwanadi wagombea wa mitaa ya Kombezi (Kata ya Makorora), Azimio (Kata ya Ngamiani Kusini), Mtambwe Kiungani (Kata ya Mnyanjani) na New Hotel (Kata ya Central).
Aidha, Ummy Mwalimu amesisitiza siku ya kupiga kura, wananchi wote waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wa CCM na yeye kama Mbunge atawapa kila aina ya ushirikiano kufanikisha utekelezaji wa ahadi zao.
Sanjari na hilo, Ummy Mwalimu amesema ana imani na wananchi wa Tanga Mjini wataichagua CCM, na deni hilo litalipwa kwa kuwaletea maendeleo katika mitaa yao.
No comments:
Post a Comment