WAZIRI MKUU na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kassim Majaliwa amewataka Wana-Liwale kuwachagua wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa Chama hicho kimechagua majembe.
Amesema kuwa kama ilivyo kwa uimara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi imara wa mwenyekiti wake, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kilichagua wagombea wazuri wenye uwezo wa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ili kuwaletea Watanzania maendeleo.
Amesema hayo leo (Jumanne, Novemba 26, 2024) wakati alipofunga kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizofanyika katika viwanja vya ujenzi, Liwale Mkoani Lindi.
“Tunawaleta hawa viongozi wapigieni kura ili wakasimamie na kuendeleza yaliyomo kwenye ilani, hawa wanaweza na ndio maana tumewaleta mbele yenu, viongozi hawa ni muhimu kwasababu watawaunganisha na viongozi wa Serikali, Sina Mashaka na Wagombea wetu”
Amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mafanikio makubwa yamepatikana kwa kuzingatia matarajio ya wananchi kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji, Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Miundombinu, Nishati na Mawasiliano.
Ameongeza kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti Dkt. Samia kwa kutambua umuhimu wa sekta ya miuindombinu, inakamilisha taratibu za ujenzi wa Barabara ya ya Masasi – Nachingwea – Liwale (175km) kwa kiwango cha lami
Wakizungumza katika mkutano huo, wagombea wa nafasi za Uenyekiti wa vijiji, vitongoji na wajumbe wa Serikali za vijiji wamewataka wananchi kuwachagua wagombea wote wanaowakilisha Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi huo kwa wana uwezo na wanania ya dhati ya kusaidiana nao kuleta maendeleo
No comments:
Post a Comment