November 20, 2024

NAIBU WAZIRI MHE.SANGU ARIDHISHWA NA USIMAMIZI BORA WA FEDHA ZA TASAF MKOANI RUKWA

Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na  walengwa wa Mradi wa TASAF katika Kijiji cha Singiwe mara baada ya kukagua shamba la miti lenye ukubwa wa ekari mbili katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Aida Kenani akizungumza na walengwa kabala ya kumakaribisha Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu kuzungumza na wananchi   mara baada ya kukagua kisima cha maji ambacho kimekarabatiwa na na kikundi cha Wanufaika wa Mradi wa TASAF katika Kijiji cha Kantawa wilayani Nkasi
Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akikagua baadhi ya miti  katika  shamba la miti lenye ukubwa wa ekari mbili katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa ambalo limeanzishwa na kikundi cha Wanufaika wa Mradi wa TASAF
Baadhi ya Walengwa wa   wa Mradi wa TASAF katika Kijiji cha Singiwe wakimsikiliza . Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu mara baada ya kukagua shamba la miti lenye ukubwa wa ekari mbili katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa
Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Aida Kenani mara baada ya kukagua kisima cha maji ambacho kimekarabatiwa na na kikundi cha Wanufaika wa Mradi wa TASAF katika Kijiji cha Kantawa wilayani Nkasi
Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwa ajili ya kukagua shamba la miti lenye ukubwa wa ekari mbili katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa  katika Kijiji cha Singiwe kilichopo katika Wilaya ya Kalambo 
************
Na Lusungu Helela -Rukwa 

Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameupongeza Mkoa wa Rukwa kwa usimamizi bora wa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini kwa kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi inayowanufaisha walengwa wa mfuko huo.
 
Mhe.Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mkoani humo  ametoa pongezi hizo leo kwa nyakati tofauti wakati alipotembelea kukagua  baadhi ya miradi inayotekelezwa na TASAF    katika Wilaya Nkasi na Kalambo.
 
Ameitaja miradi hiyo inayotekelezwa na TASAF ikiwemo ujenzi wa kisima cha maji katika Wilaya ya Nkasi pamoja na uanzishwaji wa shamba la miti ya mbao Wilayani Kalambo.
 
Akizungumzia suala la ujenzi wa kisima hicho  uliogharimu zaidi ya Sh.Milioni tatu hadi kukamilika kwake  kimekuwa msaada mkubwa kwa kuwahudumia zaidi ya kaya 200 katika Kijiji cha Kantawa 
 
Kufuatia hatua hiyo Mhe.Sangu amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nkasi kuhakikisha  anawaleta wataalamu kutoka Wakala wa Maji vjijini ( RUWASA) ili waweze kukitambua na  kukiboresha zaidi kisima hicho  kwani kimeonekana kutiririsha maji katika kipindi chote cha mwaka
 
“Jambo kubwa lililonileta hapa ni kufuatilia utekelezaji wa fedha za Mradi wa TASAF , mfuko huu umekuwa na programu mbalimbali, zikiwemo zile zinazolenga kaya maskini ambazo hupokea fedha, pamoja na shughuli za kujitolea ikiwemo ujenzi wa hiki kisima ambapo nimefarijika mno kujionea jinsi wananchi wanavyoisaidika kupitia kisima hiki" amesisitiza Mhe. Sangu 
 
Katika hatua nyingine, Mhe.Sangu amepongeza mradi wa upandaji  miti ya mbao lenye ukubwa wa ekari mbili  uliogharimu kiasi cha Sh.milioni saba  hadi kukamilika kwake ambapo mbali na  miti hiyo kutarajiwa  kutoa mbao ila kwa sasa eneo hilo limekuwa kivutio kikubwa,  achilia mbali hewa safi inayotokana  na miti hiyo 
 
Hata hivyo licha ya kupandwa jumla ya miche 2250 katika shamba hilo, Mhe.Sangu ametoa wito kwa Mkuu wa Wilaya , Mhe.Dkt. Lazaro Komba kuwaleta wataalamu kutoka Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS) ili waweze kubaini  chanzo cha tatizo kwani baadhi ya miche imeanza kunyauka.
 
Awali Mbunge wa Kalambo, Mhe. Josephat  Kandege amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha fedha za TASAF zinawafikia walengwa na kuboresha maisha yao.
 
Baadhi ya wanufaika wa TASAF  wameeleza jinsi mpango huo ulivyowawezesha kuboresha maisha yao, ikiwemo kujenga nyumba, kusomesha watoto, na kushiriki katika shughuli za maendeleo.
 
Hata hivyo,Mhe.Sangu amefafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameanzisha mpango wa mikopo yenye riba nafuu kwa vikundi vya wanufaika wa Tasaf, hatua inayolenga kuwawezesha kiuchumi zaidi.

No comments:

Post a Comment