November 11, 2024

KATIBU WA BUNGE AKABIDHI NAFASI YA MWENYEKITI MKUTANO WA MAKATIBU WA BUNGE WA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA KATIBU WA BUNGE LA KENYA

Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akishikana mkono na Naibu Katibu wa Bunge la Kenya Ndugu Jeremiah Ndombi mara baada ya kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Bunge la Kenya. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Makatibu unaofanyika Nairobi Kenya.
Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akiwa pamoja na Naibu Katibu wa Bunge la Kenya Ndugu Jeremiah Ndombi mara baada ya kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Bunge la Kenya. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Makatibu unaofanyika Nairobi Kenya.
Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akizungumza katika Mkutano wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya kwa Bunge la Kenya. Mkutano  huo wa Makatibu unafanyika Jijini Nairobi Nchini Kenya.
Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya kwa Bunge la Kenya. Mkutano  huo wa Makatibu unafanyika Jijini Nairobi 
Nchini Kenya.
*************

Katibu wa Bunge, Ndugu Baraka Leonard amekabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge Wanachama wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Katibu wa Bunge la Kenya.

 

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Makatibu wa Bunge wa EAC unaofanyika Nairobi, Kenya.

 

Akitoa hotuba ya kukabidhi nafasi hiyo, aliwashukuru Makatibu wa Bunge kwa kumpa ushirikiano ndani ya kipindi kifupi tangu alipoteuliwa kushika nafasi ya Katibu wa Bunge la Tanzania.

 

Pamoja na kushukuru kwa mapokezi mazuri kutoka kwa Mwenyeji wa Mkutano huo ambaye ni Bunge la Kenya, Katibu wa Bunge aliishukuru Sekretarieti ya Mkutano huo ambao ni Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa maandalizi mazuri ya Mkutano.

 

Alimpongeza Katibu wa Bunge la Kenya ambaye kwa niaba yake alikuwepo Naibu Katibu wa Bunge, Jeremiah Ndombi kwa kuchukua nafasi ya Mwenyekiti na kumtakia kila la heri.

 

Aidha, aliwahakishia Makatibu ushiriki wa Tanzania katika Michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuimarisha mtangamano wa Jumuiya.

 

Katibu wa Bunge pia alisisitiza umuhimu wa lugha ya kiswahli kutumika katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Mkutano wa Makatibu wa Bunge unatangulia kabla ya Mkutano wa Maspika utakaofanyika Novemba 13, 2024 ambapo pia Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhehimiwa Dkt. Tulia Ackson atakabidhi nafasi hiyo kwa Spika wa Bunge la Kenya.

No comments:

Post a Comment