Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujazaji wa fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa njia ya kielektroniki yaliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Menejimenti na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma.Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amewasisitiza
watumishi wa umma kote nchini kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo ili
kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
**************
Katibu Mkuu Mkomi ameyasema hayo leo
tarehe 21.11.2024 ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma
akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.
Amesema watumishi wanatumia muda mwingi
sana sehemu za kazi kuliko nyumbani hivyo ni vizuri wakaishi kwa upendo na
mshikamano ili kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi.
Ameongeza kuwa sehemu ya kazi ambayo
haina upendo na ushirikiano kunakuwa hakuna amani na matokeo yake watumishi
hushindwa kufanya kazi kwa ufasaha.
“Mahali pa kazi ndio sehemu ya kujenga
upendo na kuleta amani kwa watumishi wote kwani tusipofanya hivyo tutashindwa
kuwahudumia wananchi kikamilifu na kurudisha nyuma maendeleo ya taifa letu.”
Bw. Mkomi amesisitiza.
Katibu Mkuu Mkomi ametumia fursa hiyo ya
kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kwa kuwashukuru Viongozi, Menejimenti na Watumishi
wote wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa
upendo na ushirikiano ambao wamekuwa wakimpatia katika utekelezaji wa majukumu
yake.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amempongeza katibu Mkuu
Mkomi kwa kuongeza mwaka mwingine katika utumishi wa umma na kuwahamasisha
watumishi wa umma wote nchini kufanya kazi kwa umoja jambo ambalo linaleta
amani na upendo katika maeneo ya kazi kama ilivyo kwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi
wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bw. Musa Magufuli, amempongeza Katibu Mkuu Mkomi kwa kuongeza mwaka
mwingine na kuahidi kuendeleza upendo na mshikamano kwa watumishi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI
No comments:
Post a Comment