Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu amekutana na kuzungumza na Rais wa Comoro Mheshimiwa Azali Assoumani na kupokea ujumbe maalum wa Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Rais Azali Assoumani alipokutana naye jijini Moroni.
Akizungumza na Balozi Yakubu baada ya kumkabidhi ujumbe huo maalum wa Rais Samia Mhe. Rais Azali Assoumani ameelezea kuridhishwa kwake na ushirikiano wa sekta za biashara na kijamii uliopo kati ya Tanzania na Comoro.
Mhe. Rais Azali pia alimueleza Balozi Yakubu kuwa amekutana na Marais wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi; Hayati Benjamin Mkapa; Mhe. Jakaya Kikwete; Hayati John Magufuli na sasa Rais Samia Suluhu Hassan na wote wameonesha upendo mkubwa kwa Comoro na anafurahi sasa kampuni za Tanzania zinakwenda kuwekeza Comoro.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Yakubu amemshukuru Mhe. Rais Azali kwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa mamlaka mbalimbali nchini Comoro na hivyo kurahisisha utendaji kazi wake na kumueleza namna uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Comoro unavyoimarika katika siku za hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment