October 24, 2024

WAZIRI MKUU AKUTANA BALOZI WA BELARUS NCHINI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipeana mkono na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin, kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam Oktoba 24. 2024. 
***********
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 24. 2024 amekutana na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin, katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Majaliwa amemweleza Balozi Pavel kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Belarus katika Sekta za Madini, Afya, Utalii, Kilimo na Biashara kwa faida ya nchi zote mbili.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin, katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam Oktoba 24. 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin, kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam Oktoba 24. 2024. 

No comments:

Post a Comment