WASHIRIKI 280 KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA MABUNGE NCHI WANACHAMA WA CPA KANDA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika Ndugu Daniel Eliufoo akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha kuhusu Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kanda hiyo utakaofanyika Jijini Arusha tarehe 1-6 Oktoba, 2024. *************
Zaidi ya Washiriki 280 kutoka
Mabunge Wanachama wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika
watanaratajia kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 53 utakaofanyika kuanzia
tarehe 1 hadi 6, Oktoba Jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa
habari Jijini Arusha, Katibu Msaidizi wa CPA Kanda ya Afrika, Ndugu Daniel
Eliufoo alisema hadi sasa Mabunge 14 kati ya 19 yameshathibitisha kushiriki
Mkutano huo ikewemo Bunge la Tanzania.
Aidha, alisema Maspika wa
Mabunge ya Kitaifa waliothibitisha kushiriki Mkutano huo hadi sasa ni 10 na
Manaibu Spika watatu pamoja na Manaibu Spika takribani 10 kutoka katika Mabunge
ya Majimbo.
Alisema ufunguzi rasmi wa
Mkutano huo utafanyika tarehe 3 Oktoba, 2024 na Mgeni Rasmi atakuwa ni Makamu
wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ambaye atamuwakilisha Mheshimiwa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Alisema CPA Kanda ya Afrika
imekuwa ikifanya mikutano yake mikuu ya kila mwaka kwa lengo la kujadili mambo
mbalimbali kwa kuzingatia malengo ya
kuanzishwa kwa umoja huo.
“Lengo la kuanzishwa kwa Chama
cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya Madola ni kuchagiza amani, demokrasia,
uwajibikaji na haki za binadamu miongoni mwa nchi wanachama.
“Mkutano huu wa CPA – Kanda ya
Afrika ni jukwaa muhimu la kuwakutanisha washiriki mbalimbali kwa lengo la
kujadili masuala yanayowahusu kwa kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwake .” alisema.
Alisema pamoja na mkutano mkuu
wa mwaka, CPA imekuwa ikiandaa semina na mafunzo kwa lengo la kubadilishana
uzoefu na pia imekuwa ikiandaa machapisho mbalimbali.
CPA ilianzishwa mwaka 1911
ikiwa na Kanda tisa ikiwemo Kanda ya Afrika ambayo ina wanachama 19 wa Mabunge
ya Kitaifa na 64 wa Mabunge ya Majimbo.
No comments:
Post a Comment