September 21, 2024

SINGIDA WAANDAA BONANZA LA UCHAGUZI

 Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mhe.Halima Dendego amezindua bonanza la uchaguzi Mkoani humo leo jumamosi (Septemba 21,2024)yanayofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida,Kata ya Mtinko katika viwanja vya Shule ya Msingi Malolo.
Bonanza hilo limehuduriwa na viongozi mbalimbali aliwemo Katibu Tawala wa Mkoa Dkt.Fatuma Mganga,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mhe.Martha Mlata,Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mhe.Ramadhani Ihondo,Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe.Godwin Gondwe,Diwani wa Kata ya Mtinko Yusuph Bilal na wengineo.
Bonanza hilo linajumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,kufukuza kuku,kuvuta Kamba,kukimbia kwenye gunia na mingine mingi kwa lengo kubwa la kuhamasishaushiriki wa wananchi katia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika  Novemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment