September 29, 2024

SAO HILL YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI KILOSA MUFINDI

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt Linda Salekwa amewashukuru TFS kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika uendelezaji wa miradi mbalimbali kwa wananchi kwani wamekuwa wakifanya hivyo katika maeneo tofauti tofauti katika Wilaya ya Mufindi.Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt Linda Salekwa amewashukuru TFS kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika uendelezaji wa miradi mbalimbali kwa wananchi kwani wamekuwa wakifanya hivyo katika maeneo tofauti tofauti katika Wilaya ya Mufindi.
Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Saohill PCO. Tebby Yoramu amemshukuru Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Prof Dos Santos Silayo kwa kuridhia ofisi ya Shamba la Miti Saohill kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Ofisi na ukumbi wa kijiji, madarasa pamoja na jengo la utawala la shule ya msingi Kilosa.
Na Fredy Mgunda, Iringa Mufindi
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS-kupitia Shamba la Miti Saohill umekabidhi vifaa vya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika Kijiji cha Kilosa Mufindi katika Kata ya Ihanu Wilayani Mufindi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt Linda Salekwa amewashukuru TFS kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika uendelezaji wa miradi mbalimbali kwa wananchi kwani wamekuwa wakifanya hivyo katika maeneo tofauti tofauti katika Wilaya ya Mufindi.

Ameongeza kuwa Kata ya Ihanu ni miongoni mwa kata zinazonufaika sana na uwepo wa Shamba la Miti Saohill kwani awali walijengewa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ihanu lenye thamani ya zaidi ya Millioni Mia Moja, miondombinu ya barabara pamoja na utunzaji wa mazingira kwa kupata miche bure na kiupanda kwenye hekari 50.

Aidha ameuagiza uongozi wa kata na kijiji cha Kilosa kuhakikisha kuwa vifaa vilivyotolewa vinatumika kwa usahihi katika malengo ambayo yalipangwa kutekelezwa ikiwa ni ukarabati wa ofisi na ukumbi wa mikutano wa kijiji, madarasa pamoja na jengo la utawala katika Shule ya Msingi Kilosa.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Saohill PCO. Tebby Yoramu amemshukuru Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Prof Dos Santos Silayo kwa kuridhia ofisi ya Shamba la Miti Saohill kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Ofisi na ukumbi wa kijiji, madarasa pamoja na jengo la utawala la shule ya msingi Kilosa.

"Shamba la miti Sao Hill linatambua umuhimu wa mazingira bora ya kutolea huduma kwa wananchi na elimu bora kwa vijana wa kitanzania, kufuatia umuhimu huo, Shamba litakabidhi mifuko 200 ya saruji kutimiza ahadi yake ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya Kijiji" alisema PCO Tebby Yoramu

Aidha ameongeza kuwa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na jengo la utawala viko kwenye mchakato wa kununuliwa na vitawasilishwa mapema ndani ya mwaka huu na ni imani ya Shamba kuwa vitatumika ipasavyo.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano katika shughuli za ulinzi wa msitu dhidi ya majanga ya moto hususani katika kipindi hiki cha kiangazi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ihanu Michael Kiliwa ameshukuru TFS kupitia Shamba la miti Saohill kwa kuendelea kuwa msaada mkubwa katika kata hiyo kwani wamekuwa wakinufaika na miradi mbalimbali hususani katika sekta ya elimu na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

Makabidhiano hayo yamefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwepo Afisa Tawala wa Wilaya Robert Kileo, Mwenyekiti wa CCM wilaya George Kavenuke, Wahifadhi kutoka TFS, viongozi na wananchi wa kijiji cha Kilosa Mufindi.

No comments:

Post a Comment