September 19, 2024

DODOMA WAKUTANA KUJADILI STAKABADHI GALANI





Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Septemba 17,2024 ameongoza kikao kazi kwa lengo la kujadili Stakabadhi galani kutokana na mwongozo wa Biashara ya mazao ya Dengu, Mbaazi,Soya na ufuta toleo la tatu la mwaka 2024 lililotolewa chini ya Mamlaka ya udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA ) .

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Jengo la Mkapa.

Akizungumza na washiriki wa kikao hicho Mhe. Senyamule amesema lengo la stakabadhi galani ni kuhakikisha hali ya masoko na kipato cha Mkulima inaimarika kupitia uzalishaji wa mazao yenye ubora na yaliyoongezwa thamani ili kukidhi mahitaji ya soko pamoja na kuweka mifumo imara ya masoko.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wakurungezi watendaji wa Halmashauri,wakuu wa Wilaya ,Maafisa ushirika na Maafisa kilimo wa Wilaya na Mkoa wa Dodoma. 

No comments:

Post a Comment