September 22, 2024

BUNGE LATOA ELIMU KWA WANAFUNZI KIGOMA

Afisa wa Bunge, Ndugu Zuhura Mtatifikolo akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kipampa, Magongo Mayala vitabu na majarida mbalimbali kuhusu Bunge wakati Timu ya Mafisa wa Bunge walipotembelea shule hiyo pamoja na Shule ya Msingi  Kipampa zilizopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa lengo la kutoa elimu kuhusu  Bunge na majukumu yake
Afisa wa Bunge, Ndugu Omary Machunda akiwafundusha wanafunzi wa Shule ya Msingi  Kipampa na Shule ya Msingi Rusimbi zilizopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kuhusu Mhimili wa Bunge na Majukumu yake wakati timu ya Maafisa wa Ofisi ya Bunge walipotembelea shule hizo katika kutekeleza Programu yake ya Elimu kwa Umma kuhusu Bunge.
Afisa wa Bunge, Ndugu Zuhura Mtatifikolo akiwafundusha wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rusimbi iliyopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kuhusu Mhimili wa Bunge na Majukumu yake wakati timu ya Maafisa wa Ofisi ya Bunge walipotembelea shule hiyo katika kutekeleza Programu yake ya Elimu kwa Umma kuhusu Bunge.

No comments:

Post a Comment