August 16, 2024

WAZIRI KIKWETE ATETA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAAJIRI - ATE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Ndomba Doran aliyeongozana  na Meneja wa Kanda ya Kati wa ATE, Bw. Leonard Mapha alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, leo mchana, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika Wizara hiyo. 




No comments:

Post a Comment