July 07, 2024

MAPISHI,BURUDANI NA MIJADALA VYANOGESHA SIKU YA KISWAHILI COMORO








Watanzania waishio nchini Comoro na wananchi wa Kisiwa cha Ngazija na wanadiplomasia wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani kwa burudani mbali mbali pamoja na mijadala.

Takribaj washiriki 500 wamejitokeza katika Ukumbi wa Bunge la nchi hiyo ambapo nyimbo za kitanzania,mashairi na maigizo vilipamba shughuli hiyo.

Aidha,mapishi mbali mbali ya asili ya pwani yalinogesha shughuli hiyo iliyoambatana pia na mjadala wa kisomi kuhusu changamoto na maendeleo ya Kiswahili nchini Comoro ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja,Ibrahim Mze.

Awali,Balozi wa Tanzania nchini humo aliwasilisha ombi kwa Gavana huyo kuwa Comoro ina kila sababu ya kurasimisha matumizi ya Kiswahili kuwa lugha rasmi kwa kuzingatia historia ya visiwa vyake na Ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na kuainisha faida nyingi za Kiswahili.

Naye Gavana Mze katika hotuba yake alisema wananchi wengi wa Comoro wana historia na asili ya Tanzania na hivyo ni vyema Ubalozi urasimishe ombi hilo ili kuongeza matumizi ya Kiswahili ambapo alifurahi kuona watoto wa shule na vyo vikuu wakishiriki maadhimisho hayo.

Sherehe za Maadhimisho hayo zilihudhuriwa na waalikwa mbalimbali ikiwemo Mheshimiwa GUO ZHIJUN, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Comoro; Bw. James Tsok BoT, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa; Bi. Nichola SABELO, Kaimu Mkuu wa Kituo, Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Comoro; Bw. Youssouf Ali, Mshauri wa Rais wa Comoro masuala ya Elimu, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Urafiki kati ya Tanzania na Comoro; Bw. Abdillah M’Saidie, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Sanaa; pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini Comoro na wamiliki wa vyombo vya habari vinavyotangaza Kiswahili nchini Comoro.

Ratiba ya Maadhimisho hayo ilihusisha kugawa zawadi kwa washindi wa Shindano la Uandishi wa Insha lililoratibiwa sambamba na maadhimisho hayo. Washiriki wasipoungua 20 walishiriki Shindano hilo. 

Aidha, hadhira ilipatiwa fursa ya kuona picha jongefu ikiwa na ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili mwaka 2024.  

Kwa kipekee,Balozi Yakubu aliahidi kuwa Ubalozi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali muhimu ili wataanzisha darasa la kufundisha somo la Kiswahili nchini Comoro, pamoja na kuhamasisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na waandishi wa habari kutoka Tanzania na Comoro. 

Katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili nchini Comoro, Ubalozi uliratibu wiki ya mswahili kuanzia tarehe 4 – 6 Julai, 2024 ambapo matukio mbalimabali yalifanyika ikiwemo Kilele cha Sherehe hizo kilichotangaza washindi wa zawadi mbali mbali ikiwemo tiketi ya kwenda Tanzania iliyotolewa na Shirika la Ndege la Tanzania,ATCL.

Comoro haiko nyuma katika ufundishaji wa somo la Kiswahili. Taasisi mbalimbali za elimu zinazofundishs somo la Kiswahili ikiwemo Kitivo cha Teknolojia cha Chuo Kikuu Comoro, Shule ya Msingi na Sekondari Mwinyi Baraka, Shule ya AIMECEZER, Shule ya IBNU SIRIN, Taasisi ya Elimu EZAG, pamoja na Kituo cha lugha cha STAR English walishishiriki maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment