July 08, 2024

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU - DHIBITI RUSHWA KWENYE MANUNUZI YA UMMA KWA KUTUMIA MFUMO WA NeST


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Godfrey Mnzava akikata utepe kuashiria kufungulia kwa barabara ya lami yenye Urefu wa Kilomita 1.21 ya Minga - Imbele katika Manispaa ya Singida ambayo imejengwa kwa Gharama ya zaidi ya shilingi milioni 992.
Meneja wa Tarura Manispaa ya Singida Mhandisi Lazaro Kitomary akieleza jinsi mradi wa barabara ya Minga - Imbele  jinsi ulivyotekelezwa.

Maelezo kwa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kuhusu jinsi mradi wa barabara ilivyotekelezwa.
**********
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amewaagiza Viongozi wa Mikoa na wilaya nchini kutumia Mfumo mpya wa Kielekroniki wa Manunuzi wa Umma -NeST - kama hatua ya kupata Wakandarasi bora na kudhibiti Vitendo vya Rushwa kwenye uombaji wa zabuni.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ametoa kauli hiyo ‎(08-‎Jul-‎2024) wakati anazindua barabara ya lami yenye Urefu wa Kilomita 1.21 ya Minga - Imbele katika Manispaa ya Singida ambayo imejengwa kwa Gharama ya zaidi ya shilingi milioni 992.

Mnzava amesema mfumo wa NeST ni salama ni wa wazi kwa sababu kila mchakato wa manunuzi wa umma  unaofanyika ndani ya mfumo kila mwombaji aliyepewa dhamana ya kuingia kwenye mfumo huo anaona au anajua kinachoendelea kwenye mchakato huo hali ambayo inapunguza vitendo vya rushwa wakati wa mchakato huo.

"Mhe Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kuona mfumo huo NeST unatumika ipasavyo kwa ajili ya kudhibiti manunuzi ya umma, Amesisitiza Mnzava.

Ameeleza kuwa mfumo huo umeundwa na Wazawa na una asilimia kubwa ya kulinda siri na usalama wa nyaraka za Serikali ukilinganisha na mfumo wa TANeMPS uliokuwa chini ya wageni. 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amesisitiza kuwa mfumo huo hauna upendeleo kwa sababu kila mwombaji wa zabuni anaona eneo gani amefaulu na eneo ambalo hajakidhi vigezo. 

Mfumo Mpya wa Kielekroniki wa Manunuzi ya Umma - National -e- Procurement System - NeST unatarajiwa kuwa mbadala wa Mfumo wa awali wa manunuzi ya umma uliojulikana kama Tanzania National -e- Procurement System yaani TANePS.

Akisoma Taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa Mkimbiza Mwenge Uhuru, Meneja wa Tarura Manispaa ya Singida Mhandisi Lazaro Kitomary amesema ujenzi wa barabara hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa shughuli za usafiri na usafirishaji kwa wakazi wa maeneo hayo.


PTC 1. 

PTC 2. Sehemu ya barabara iliyojengwa ya Minga - Imbele katika Manispaa ya Singida.

PTC 3. 
PTC 4- 5 - .

No comments:

Post a Comment