Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3 , hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso Mkoani Mtwara .Dkt Nchimbi ametembelea kaburi hilo Leo Julai 28, 2024. na kutoa Pole kwa familia na kuzungumza na Wananchi wa Lupaso.
Balozi Nchimbi amesema "naomba nikiri kuwa Mimi ni mwanafunzi wa hayati na nimekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa katika kipindi Chake kwani ndio alinilipia Ada ya kusoma Chuo kikuu na alikuwa mfuatiliaji sana na alitulea na sio Sisi lakini kwa Watanzania wote aliwalea pia alikuwa mzalendo kwa Nchi alifanya mabadiliko Makubwa kwa Nchi yake na Kwa Chama Chake lakini yote CCM chini ya Dkt Samia tutaendelea kuyaenzi Yale yote aliyoyoacha Hayati Benjamin Mkapa na pamoja hayo nimeambiwa kero za hapa na tumezichukua lakini CCM inatoa Shilingi Milioni 10 kuanza kukarabati Shule ya hapa Lupaso".
Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.
No comments:
Post a Comment