Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amefungua maonesho ya Utalii ya _Karibu Kili Fair_ yanayofanyika katika Viwanja vya Magereza Kisongo Mkoani Arusha na kuhamasisha wanachi kupigia kura vivutio vya utalii vilivyoingia katika kinyang'anyiro cha tuzo la _World travel a_ wards kwa mwaka 2024.
Akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas, Mhe. Kairuki ametembelea banda la NCAA na kujionea shughuli za utoaji elimu na maelezo kuhusu Utalii, uhifadhi na maendeleo ya Jamii zinazofanyika katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Katika banda la NCAA Waziri Kairuki alitumia muda huo kuwahamasisha wageni waliotembelea maonesho hayo kupigia kura vivutio vya utalii ambapo eneo la hifadhi ya Ngorongoro linawania tuzo ya kuwa kivutio bora cha Utalii barani Afrika kwa mwaka 2024.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro lilishinda tuzo hiyo mwaka 2023 na mwaka huu linawania tuzo hiyo ambapo hatua za upigaji kura ni kama ifuatavyo 👇👇
1.Tembelea tovuti ya www.worldtravelawards.com/vote
2. Jisajili kwa kufuata hatua zote
3. Fungua Barua pepe yako uliyojaza ili kufanya uthibitisho
4. Chagua bara la Afrika, piga kura kwenye kipengele cha Africa’s Leading Tourist Attraction na chagua Ngorongoro Conservation Area
Kura Yako, Ushindi Wetu!
No comments:
Post a Comment