June 20, 2024

TEKNOLOJIA ZA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MIRADI YA MAJI ZAJADILIWA CHINA







Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso anashiriki Kongamano la Kumi na Tano la Uwekezaji katika Ujenzi wa Miundombinu (15th International Infrastructure Investment and Construction Forum and Expo) linalofanyika tarehe 19-21 Juni, 2024, Macao SAR, China.


Mhe. Aweso ameshiriki katika mdahalo kuhusu teknolojia za ujenzi wa miundombinu inayohimili mabadiliko ya tabianchi na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa.


Akizungumza katika mdahalo huo na kutoa mifano ya miundombinu ya maji, Mhe. Aweso amebainisha kuwa kwa sasa sehemu kubwa ya kazi ya usambazaji maji nchini Tanzania zinahusisha ujenzi wa miradi yakiwemo matanki na mabwawa.

Katika muktadha huo, amikaribisha Jumuiya ya Kimataifa na kwa namna ya pekee nchi ya China kushirikiana na Wizara ya Maji katika ujenzi wa Gridi ya Maji ya Taifa, Ujenzi wa kiwanda cha mita za maji za malipo ya kabla na uboreshaji wa teknolojia za kudhibiti mivujo ya maji.

Wizara ya Maji Tanzania ni miongoni mwa Sekta zilizoalikwa kushiriki katika Kongamano hilo linalohusu uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu inayozingatia usimamizi wa mabadiliko ya tabianchi.

No comments:

Post a Comment