February 02, 2024

MZEE MWINYI ALAZWA KWA MATIBABU

TAARIFA KWA UMMA
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi  amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua. 

Anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari. 

Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali.

Abdullah Ali Mwinyi 
Msemaji wa Familia

1 comment:

  1. Amiin...Allah amuondoshee maradhi na ampe umri zaidi!

    ReplyDelete