January 07, 2024

KAMPUNI YA LAKE ENERGIES YAWAFARIJI WA HANGA WA MAFURIKO HANANG

Mkuu Wa Wilaya Ya Hanang Mkoa wa Manyara,Bi. Janeth Mayanja (kulia) akikabidhiwa msaada wa mtungi wa gesi kati ya mitungi (100) na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies,Matina Nkurlu (kushoto)  pamoja na vifaa mbalimbali vya matumizi ya manyumbani kwa ajili ya wahanga wa mafuriko mkoani humo vilivyotolewa na Kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Anayeshuhudia katikati ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo kanda ya kasikazini,Ismael Juma.
Mkuu Wa Wilaya Ya Hanang Mkoa wa Manyara,Bi. Janeth Mayanja (kulia) akikagua moja ya ndoo ya kunawia mikono aliyokabidhiwa msaada na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group, Matina Nkurlu (kushoto) pamoja na mitungi ya gesi yakupikia (100) na vifaa mbalimbali vya matumizi ya manyumbani kwa ajili ya wahanga wa mafuriko mkoani humo vilivyotolewa na Kampuni hiyo mwishoni mwa wiki.
Mkuu Wa Wilaya Ya Hanang Mkoa wa Manyara,Bi.Janeth Mayanja (katikati) akipokea  msaada wa mfuko wa sabuni yakufulia toka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group, Matina Nkurlu (kushoto) pamoja na mitungi ya gesi yakupikia(100)na vifaa mbalimbali vya matumizi ya manyumbani kwa ajili ya wahanga wa mafuriko mkoani humo vilivyotolewa na Kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo kanda ya kasikazini,Ismael Juma.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Lake Energies,Matina Nkurlu(kushoto)akimfafanulia jambo Mkuu Wa Wilaya Ya Hanang Mkoa wa Manyara,Bi. Janeth Mayanja,wakati wa kumkabidhi msaada wa mitungi ya gesi yakupikia(100)pamoja na vifaa mbalimbali vya matumizi ya manyumbani kwa ajili ya wahanga wa mafuriko mkoani humo vilivyotolewa na Kampuni hiyo mwishoni mwa wiki.

Wafanyakazi wa  Lake Energies wakiongozwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu, walifika wilaya ya Hanang, mkoani Manyara na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Bi Janeth Mayanya na kumkabidhi msaada wa mitungi ya gesi 100 na vifaa vingine mbalimbali vya matumizi ya nyumbani kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wa wilaya hiyo mkoani manyara. Msaada huo umetolewa takribani mwezi mmoja baada ya mafuriko makubwa yaliyotokea wilayani humo.

No comments:

Post a Comment