January 21, 2024

FANYENI BIRTHDAY KWA KUPANDA MITI KULINGANA NA UMRI WAKO










Katika kuhakikisha Taifa linakabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi  wananchi  wametakiwa kupanda miti kwa wingi hasa wanaposherekea siku zao za kuzaliwa

Hayo yamesemwa na  Brigedia Jenerali Mstaafu Martin Amos Kemwaga ambaye pia ni Mkurugenzi wa MAKMar Hotel iliyopo katika Kata ya Msata Wilayani ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambaye pia ni mwasisi wa kampeni ya “MITI KWA UMRI”-KIJANI KIRUDI  Wakati akisherekea siku yake ya kuzaliwa mapema January 20, mwaka 2024

Kemwaga amesema ameanzisha kampeni inayoitwa "MITI KWA UMRI"-KIJANI KIRUDI

Akiwa na maana kila Mtanzania anaposherekea siku yake ya kuzaliwa ahakikishe anapanda miti sawa na umri wake Ili Tanzania iwe ya kijani
“Nimeamua kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwangu kwa kupanda miti sawa na umri wangu ili kutekeleza Kampeni ambayo niliiasisi tarehe 7/10/2019 na kuzinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. 

Nimeona ni vyema kuendelea kuitambulisha kampeni hii ili  watanzania  waweze kuielewa na kuitekeleza. 

"Kwa kifupi miti kwa umri ni kupanda miti kulingana na umri wako mfano; kama una umri wa miaka 40 utapanda miti 40,  mwaka ujao utapanda miti 41 kwa kufanya hivyo ninaamini Tanzania itakuwa ya kijani,  kikubwa katika hili miti utakayopanda siku ya kuzaliwa kwako utakuwa unawajibika nayo, tumeona miti mingi ikipandwa lakini haina utunzaji  matokeo yake inakauka,".  

"Lakini tukitumia birthday zetu ambazo tunapenda tule vizuri, tuvae vizuri zitatukumbusha kutunza miti tuliyoipanda kama tunavyo zihangaikia birthday zetu aidha kila ukipanda mti utakuwa umeweka alama itakayokutambulisha na kurithisha wengine. Sote tutambue kwamba miti ndiyo mapafu ya duania kwa hiyo kuna umhimu wa kupanda miti tunaposherekea siku zetu za kuzaliwa, ili Dunia iweze kupumua ” alisema Brigedia Jenerali Msltaafu Martin Amos Kemwaga.

Mwasisi wa kampeni hii pia amebaisha kuwa kuanzia mwaka huu atapanda miti kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Marais wa awamu zote.

Moja ya mwanachi  aliyejitokeza kusherekea siku ya kuzaliwa kwa Bregedia Jenerali Kemwaga Ndg. Nipul Laxman kutoka Kampuni Z&A Investment LTD amesema “ tumejumuika kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa ndugu yetu Martin Amos Kemwaga  na tunashiriki kupanda miti kama moja ya sehemu ya kusherekea,  kumpongeza na kumuunga mkono kwa Kampeni aliyoisisi ya “MTI KWA UMRI”-KIJANI KIRUDI  tutahakikisha tunamuunga mkono na sisi kwenye Birthday zetu” alisema Laxman

Kwa Upande wake David Ntemi Mhifadhi Misitu  TFS Halmashauri ya Chalinze amesema  wao kama Serikali wamepongeza kuanzishwa kwa kampeni  hiyo na wametoa miche 250 kuunga mkono mkono  Kampeni ya “MITI KWA UMRI”–KIJANI KIRUDI. Aidha Mhifadhi Misitu amewataka wakazi wa Chalinze na Watanzania kwa ujumla kuiga kampeni hiyo pia amesema miche ya miti inatolewa bure na Wakala wa Huduma za Misitu TFS hivyo wananchi wanaposherekea matukio mbalimbali wapande miti ili kuhakikisha Tanzania kijani kinarudi. 

No comments:

Post a Comment