December 05, 2023

WANAFUNZI WAAPA KUTO KAA KIMYA KUTOA TAARIFA ZA UKATILI DHIDI YAO

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP .Theopista Mallya akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nambala iliyopo Mbozi mkoani Songwe.

Na Issa Mwadangala
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nambala iliyopo Mbozi mkoani Songwe, wameapa kamwe hawatakaa kimya kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto kwenye maeneo yao na kufichua ukatili wanaofanyiwa nyumbani, njiani na mtaani kwani Polisi ni marafiki zao.

Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo Disemba 04, 2023 baada ya kupata elimu na kujengewa uelewa kuhusu umuhimu wa kuwa karibu na Polisi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za ukatili na vitendo vingine vya kihalifu.

Elimu hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP .Theopista Mallya ikiwa ni muendelezo wa dhana ya ushirikishwaji wa jamii kwa makundi yote kwa lengo la kufichua na kudhibiti uhalifu mkoani Songwe.

Aidha, Kamanda Mallya aliwasihi wanafunzi hao kuacha kupokea zawadi kwa watu wasiowafahamu pia kukataa kutumwa na watu wasiowafahamu ikiwemo kuacha kudhulura hovyo na kutembea usiku wakiwa peke yao ili kuepuka kufanyiwa vitendo vya ukatili.

No comments:

Post a Comment