Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka, kabla ya Ibada Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Onaeli Shoo kabla ya Ibada ya Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka katika Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo Desemba 5, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Akiaga Mwili wa Marehemu Baba Askofu Mstaafu Dkt. Erasto Kweka, wakati wa Ibada Maalum ya Kuaga Mwili leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Onaeli Shoo kabla ya Ibada ya Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka katika Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo Desemba 5, 2023.
************
Na Mwandishi wetuNaibu Waziri Mkuu na Waziri
wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa
wito kwa viongozi mbalimbali serikalini kuhakikisha kuwa, kazi walizonazo
wanazifanya kwa bidii kubwa na kuacha alama nzuri kwa wananchi, hivyo ni muhimu kazi hizo
zikaonekana na kufaidisha wananchi.
Amesema hayo tarehe 5 Desemba 2023 wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ibada Maalum ya kuaga Mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka iliyofanyika katika Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Samia Suluhu Hassan anatambua mchango wa Marehemu Baba Askofu Kweka kwenye maendeleo ya Kanisa la KKKT na kwamba Serikali itauenzi mchango wake katika Sekta pia za Afya, Elimu na Maji.
Pia ametoa pole kwa Wananchi na Serikali kufutia maafa yaliyotokea katika Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara ambapo baadhi ya wananchi wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kufuatia maporomoko ya ardhi na ameeleza kuwa Kanisa linafarijika na juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kutatua changamoto katika eneo hilo, na tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa yupo katika eneo la maafa na timu kutoka kwenye ofisi yake.
Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto N. Kweka alizaliwa tarehe 24 Aprili, 1934 katika Kijiji cha Mamba Uswaa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambapo enzi ya uhai wake alitumika katika nyanja mbalimbali ikiwemo Ualimu, kabla ya kuingia ngazi ya Utumishi wa Kanisa.
No comments:
Post a Comment