Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambaye pia yeye na mama yake ni waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Bi. Christina
Nyangole pamoja na mtoto wake Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8
ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang Mkoani Manyara
tarehe 7 Desemba, 2023. Bi. Christina na Mtoto wake ni waathirika wa mafuriko
yaliyotokea Katesh, Hanang Mkoani Manyara.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji muathirika wa mafuriko
yaliyotokea Katesh Bi. Salome Elifuraha ambaye amelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Tumaini iliyopo Katesh, Hanang. Mama amepoteza watoto wawili kwenye
maafa hayo huku mtoto wa tatu akiwa bado hajapatikana hadi sasa. Rais Samia
aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika
hospitali hiyo ya Wilaya Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waathirika wa Mafuriko
waliopo kwenye kambi zao Katesh, Wilayani Hanang mkoani Manyara
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waathirika wa Mafuriko
waliopo kwenye kambi zao Katesh, Wilayani Hanang mkoani Manyara
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waathirika wa Mafuriko
waliopo kwenye kambi zao Katesh, Wilayani Hanang mkoani Manyara.Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.
Queen Sendiga akielezea kuhusiana na athari za mafuriko yaliyotokea katika eneo
la Jorodom Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia ametembelea eneo hilo Mkoani
Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ndugu Elibariki
Naman mkazi wa Jorodom, Katesh ambaye ni muathirika wa Mafuriko yaliyotokea
Wilayani Hanang. Ndugu Elibariki alikuwa akielezea jinsi majirani zake
walivyopoteza maisha pamoja na makazi yao katika maafa hayo
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Jorodom
ambalo limeathirika na Mafuriko pamoja na
maporomoko ya matope na mawe Wilayani Hanang Mkoani Manyara tarehe 7
Desemba, 2023. Rais Samia alijionea uharibifu mkubwa uliotokea na kuwapa pole
Waathirika wa maafa hayo na kuwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wakati wakiangalia athari za mafuriko yaliyotokea katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta wakati akiangalia
athari za mafuriko yaliyotokea katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji
jirani, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
No comments:
Post a Comment