Na Issa Mwadangala
Askari wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Theopista Mallya baada
ya ukaguzi wa paredi la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kisha kufanya
baraza na Maafisa , Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali Disemba 20, 2023.
Kamanda Mallya amewasisitiza
viongozi wanao wasimamia Askari katika kutekeleza majukumu kuhakikisha
wanatenda kwa uadilifu ili kuleta matokeo chanya na kupunguza malalamiko dhidi
ya Jeshi la Polisi.
Naye, Afisa Mnadhimu wa Polisi
Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gallas Hyera amesisitiza na
kukemea mambo kadha wa kadha yakiwemo askari kuacha kujihusisha na vitendo
ambavyo vinaleta taswira mbaya kwa Jeshi la Polisi na kuwataka kufanya kazi kwa
kufuata wimbo wa maadili ya Afisa wa Jeshi la Polisi ambao unasisitiza nidhamu,
haki, weledi na uadilifu.
Jeshi la Polisi nchini
limejiwekia utaratibu wa kukutana na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo
mbalimbali mara kwa mara katika mabaraza na vikao kazi kwa lengo la
kukumbushana majukumu ya kazi na kuweka mipanga mkakati ya utendaji kazi
ikiwemo kuzuia na kutanzua uhalifu.
Askari wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment