Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde pamoja na Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, Watendaji na Wataalam wa Wizara hizo mbili wamekutana leo Novemba 16, 2023, jijini Dar es Salaam na kufanya kikao cha pamoja kuhusu mustakabali wa Uagizwaji wa madini ya chumvi kutoka nje ya nchi.
Awali, kikao hicho kilipokea taarifa ya takwimu za chumvi zilizoko maghalani hivi sasa kwa ajili ya kutathmini hali ya uzalishaji wa chumvi nchini sambamba na kulisha viwanda vya usindikaji bidhaa hiyo.
Kikao hicho pia kilipokea taarifa ya ununuzi wa madini ya chumvi uliofanywa na kiwanda cha Neelkanth Salt Limited na kutaka kufahamu ikiwa chumvi ghafi ilifuatwa mashambani au wauzaji walipeleka kiwandani kwa ajili ya usindikaji.
Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga pamoja na Watendaji na Wataalam mbalimbali kutoka wizara zote mbili.
No comments:
Post a Comment