Hayo yamebainishwa leo Novemba 20, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa watendaji hao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Roma Complex Jijini Dodoma.
Mhe. Senyamule amesema watendaji wa Kata wanapaswa kufuata Sheria na kanuni za kiutendaji ili kuwapunguzia mzigo wa kero wananchi wa chini na sio kusubiri viongozi wa juu kufika kwenye maeneo yao kutatua kero.
"Serikali imeekeleza kila mtendaji asikilize kero na kuzitatua. Kazi kubwa ya mtendaji ni kuonesha njia kwenye Tarafa yako kwani changamoto kubwa iliyopo hapa ni mabadiliko bado ni madogo kulingana na matarajio ya Serikali.
" Mumewekwa pale kulinda heshima ya Serikali kwa kazi, maneno na matendo yenu. Jambo hili halifanyiki kwa uthabiti wa kutosha ndio maana munapewa mafunzo haya ili kuwakumbusha Sheria na kanuni mpya ili kuongeza maarifa kwa watumishi waweze kumudu majukumu yao" amesema Mhe. Senyamule.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurungenzi wa TAMISEMI Bi. Angelista Kihanga, amesema kuwa, mafunzo haya yamepewa umuhimu wa hali ya juu kwani yalianza awamu ya kwanza kwenye Mkoa wa Mbeya na Mikoa ya Magharibi na Sasa yanafanyika kwenye Mikoa ya Kanda ya kati kwa kuhusisha Maafisa Tarafa na Kata kwani ndio watekelezaji wa sera za nchi kwa wananchi.
Mafunzo kwa Maafisa wa Tarafa na Kata yaliyoandaliwa na Wizara ya TAMISEMI, yanagusia mada mbalimbali zikiwemo mwongozo wa ushughulikiaji malalamiko ya wananchi katika utumishi wa umma na huduma kwa wateja, ununuzi wa umma, nafasi ya Afisa Tarafa na Mtendaji wa Kata katika mafanikio ya Serikali, kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma na Sera na Sheria za uendeshaji wa Serikali za Mitaa.
No comments:
Post a Comment