November 18, 2023

WANAKONDOA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Novemba 18 ameshiriki Bonanza la Michezo liliondaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt .Khamis Mkanachi na kufanyikia katika viwanja vya Sabasaba Wilani Kondoa.



Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi akizungumza na kubainisha kuwa licha ya Bonanza Hilo kujikita katika kuelezea na kuonyesha mafanikio hayo ya awamu ya Sita pia ametaka Bonanza Hilo litumike Kama uwanja wa wanafunzi kumfahamu vizuri Dkt. Samia kwani ni tunu ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Novemba 18 ameshiriki Bonanza la Michezo liliondaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt .Khamis Mkanachi na kufanyikia katika viwanja vya Sabasaba Wilani Kondoa.

Bonanza Hilo lililojikita katika kuelezea Mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Hassan Suluhu, limejumuisha Michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa Miguu,kukimbiza kuku, kukuna nazi, kutembea ndani ya magunia, kuvuta kamba na shindano la kula pilipili  ambapo awali kulitanguliwa na Matembezi ya hisani yaliyoanzia katika Barabara ya Darajani Hadi viwanja vya Saba Saba Kondoa Mjini.

Akihutubia Makutano waliojitokeza Mhe. Senyamule amewaasa Wanakondoa kuendelea kudumisha Amani na Utulivu kwa kufanya matendo mema na yaliyo na tija kwa Taifa letu.

"Nitoe Shime tuendelee kuimarisha Amani na Utulivu pia tuendelee kufanya matendo mema ambayo yatapelekea nchi Yetu ya Tanzania Kuendelea kuwa na Amani kwasababu Rais wetu ametamani tupendane, tushikamane na tuwe na umoja na ameanza kuyafanya, kupishana kwenye jambo sio kufarakana mnapopishana  munakaa mezani kuangalia chanzo cha tatizo na munalimaliza Kama Watanzania," Amesema Senyamule

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Khamis Mkanachi amebainisha kuwa licha ya Bonanza Hilo kujikita katika kuelezea na kuonyesha mafanikio hayo ya awamu ya Sita pia ametaka Bonanza Hilo litumike Kama uwanja wa wanafunzi kumfahamu vizuri Dkt. Samia kwani ni tunu ya Taifa.

Aidha Dkt. Mkanachi ameweka bayana kuwa katika kipindi cha Miaka 3 ya Rais Samia madarakani Wilaya ya Kondoa imepokea Billioni 52.634 za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na yenye tija kwa Wananchi wa Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment