Kikosi kazi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara,Wizara ya Kilimo ,Ofisi ya Rais Tamisemi leo tarehe 20 Novemba,2023 kimefanya ziara na kufanya mazungumzo na Kaimu Afisa Tawala Msaidizi sehemu ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Bwana Lusungu Esau Mdede Mkoani Njombe.
Lengo la ziara hiyo kufanya tathimini ya namna bora mazao ya kilimo yanavyoweza kufungashwa kwa kufuata vipimo sahihi
Aidha, Bwana Mdede amesema ujio wa kikosi kazi hiki ni tumaini na suluhisho kwa wakulima kwani wengi wamekuwa na hamasa ya kupata. elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo kwani itasaidia katika upatikanaji wa faida zaidi na kuepukana na matumizi ya madebe na visado katika mazao ya kilimo hususani nyanya,vitunguu,karoti,tangawizi na viazi mviringo
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya maendeleo ya biashara Dkt.Hanifa Mohammed Yusuph amesisitiza kuwepo na matumizi sahihi ya vipimo katika mazao kilimo ni muhimu ili kuwezesha upatikanaji wa mapato Serikalini na kukuza ustawi wa biashara nchini
wakati huohuo wakulima na wafanya biashara mkoani Njombe wamepewa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipimo ili kuepuka hasara na pia adhabu mara watakapobainika kukikuka sheria ya vipimo nchini
kilosi kazi hiki kimeanza tathimini hii tarehe 13 Novemba,kikipitia katika masoko ya jiji la Dar es salaam,Arusha,Manispaa ya Iringa na mkoa wa Njombe kwa lengo la kutathmini ufungashaji wa mazao ya kilimo yasiyofuata vipimo sahihi
No comments:
Post a Comment