Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na kundi maalum la wawekezaji na watalii mahiri duniani zaidi ya 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine duniani wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba (kushoto) na baadhi ya wageni waalikwa wakifurahia burudani ya muziki kutoka kwa Msanii wa Singeli ,Sholo Mwamba katika hafla ya kuwaaga zaidi wa watalii na wawekezaji mahiri 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine Duniani, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo (Mb) (katikati) na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kuwaaga zaidi wa watalii na wawekezaji mahiri 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine Duniani, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.Baadhi ya Watalii na Wawekezaji mahiri kutoka Marekani na nchi nyingine duniani wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)(hayupo pichani) katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.
Mmoja wa watalii ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Marekani ya DAYBREAKER & WOW IT’S NOW ,Radha Agrawal akizungumza katika hafla ya kuwaaga zaidi wa watalii na wawekezaji mahiri 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine Duniani, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo (Mb) akizungumza katika hafla ya kuwaaga zaidi wa watalii na wawekezaji mahiri 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine Duniani, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa zawadi kwa kundi maalum la wawekezaji na watalii mahiri kutoka Marekani na nchi nyingine duniani kwenye hafla ya kuwaaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) (kushoto) wakifuatilia matukio katika hafla ya kuwaaga zaidi wa watalii na wawekezaji mahiri 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine Duniani, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa Novemba 12,2023.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amewahakikishia
kundi maalum la wawekezaji na watalii mahiri duniani zaidi ya 150 kutoka nchini Marekani na nchi nyingine duniani lililowasili nchini Novemba 4,2023 kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika jitihada za kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya utalii
Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo Novemba 12,2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Mout Meru jijini Arusha, Mhe.Kairuki amesema moja ya lengo kuu la hafla hiyo ni kuitangaza Tanzania kama kivutio cha utalii na pia soko la utalii la kuvutia na la uhakika kwa wageni wa Marekani.
“Serikali ya Tanzania inahimiza uwekezaji katika miundombinu na maendeleo ya masoko ya utalii na hii ni fursa nzuri kwa makampuni ya Marekani kuongeza mauzo na kupata maeneo ya kimkakati ya kukuza uwekezaji barani Afrika” Mhe. Kairuki amesisitiza.
Aidha Mhe. Kairuki ametumia fursa hiyo kuyakaribisha makampuni ya Marekani kushiriki katika kukuza sekta ya utalii ya Tanzania.
Amefafanua kuwa Sekta ya utalii nchini Tanzania huzalisha zaidi ya dola Bilioni 2.6 katika pato la Taifa pamoja na kutoa ajira zaidi milioni 1.5 kwa wananchi wake.
Kuhusu ongezeko la Idadi ya watalii wanaotembelea nchini Tanzania Mhe. Kairuki amesema mwaka jana ulikuwa mwaka wa rekodi kwa utalii nchini Tanzania, ambapo zaidi ya wageni milioni moja walikuja kufurahia maeneo ya ikolojia ambapo jumla watalii 100,600 walikuwa ni kutoka nchini Marekani.
Amesema ongezeko la idadi ya watalii linatokana na kuongezeka kwa utangazaji wa Utalii kupitia Filamu ya “Tanzania the Royal Tour” pamoja na matangazo ya television ya CNN ambapo vivutio vya utalii vinaendelea kutangazwa duniani kote.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kairuki amesema Tanzania itakaribisha kikundi cha wachezaji 120 maarufu wa tenisi na wapenda tenisi kutoka Marekani ambao watakuwa kwenye McEnroe Luxury Safari Tour, na Mashindano ya Tenisi yatakayofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mwezi Desemba,2023.
No comments:
Post a Comment