Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipekua jarida lenye taarifa mbalimbali za TASAF huku akisikiliza maelezo ya Bw. Shedrack Mziray Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya Taasisi za Kifedha yanayofanyika mkoani Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kushoto ni Peter Ilomo Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na wanufaika mbalimbali wa TASAF ambao ni wajasiriamali wakati alipotembelea katika banda hilo jijini Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimsikiliza Bi. Tatu Ramadhani mnufaika wa TASAF ambay ni mjasiriamali wakati alipotembelea katika banda hilo jijini Arusha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimshukuru mnufaika wa TASAF Bi. Tatu Ramadhan ambaye ni mjasiriamali mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa mjasiriamali huyo alipotembelea banda hilo.
Bw. Shedrack Mziray Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katikati akifurahia jambo na Fariji Mishael Mkurugenzi wa Tathmini na Mifumo TASAF kulia na Bi. Zuhura Mdungi Mtaalam wa mawasiliano TASAF.
Meneja wa Kuweka Akiba na Kutunza Uchumi wa Kaya Bi. Sara Mshiu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) akizungumza na mwandisi wa Fullshangwe hayupo pichani namna TASAF inavyowajengea uwezo na kuwasaidia kaya maskini kwa kutoa mafunzo na kuwaonesha fursa za kiuchumi kwa kushiriki katika maonesho mbalimbali ikiwemo Taasisi za Fedha.
NA JOHN BUKUKU, ARUSHA
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kuweka mifumo ya kuratibu vikundi vya ujasiriamali ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao wamekuwa na ufanisi mkubwa katika ujasiriamali kwa kukuza mtaji mdogo hadi kufikia kiwango cha juu.
Akizungumza leo Novemba 22, 2023 Mkoani Arusha akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tatu wa wiki ya huduma za kifedha, Mhe. Majaliwa, amesema kuwa wakati umefika kwa Kila Wilaya na Mkoa kuwatafutia masoko wajasiriamali pamoja na kubuni maonesho ambayo yataongeza wigo katika biashara.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa TASAF kuna wajasiriamali wazuri ambao wameweza kukuza mtaji mdogo waliopewa na kufanikisha kukuza mtaji na kuanzisha biashara zenye mitaji mikubwa.
"Changamoto iliyopo halmashauri zetu hazijaweza kuwaweka pamoja wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuwaelimisha na kuhamasisha kwa kutafuta maeneo kwa ajili ya kupelekea bidhaa zao" amesema Mhe. Majaliwa
Wakati huo huo Meneja wa Kuweka Akiba na Kutunza Uchumi wa Kaya Bi. Sara Mshiu amesema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeendelea kuwajengea uwezo na kuwasaidia kaya maskini kwa kutoa mafunzo na kuwaonesha fursa za kiuchumi kwa kushiriki katika maonesho mbalimbali ikiwemo Taasisi za Fedha.
amesema lengo lao ni kunusuru kaya maskini kwa kumsaidia mlengwa katika kuhakikisha wanapiga hatua.
Mshiu amesema kuwa walengwa ambao wanatoka katika kaya maskini wameshiriki katika maonesho hayo Kwa ajili ya kuonesha bidhaa ambazo wanatengeneza pamoja na kuziuza.
Amesema kuwa wamekuwa wakipewa mafunzo ya uzalishaji wa fedha kupitia bidhaa ambazo wanatengeneza.
"Tuna programu ambayo inawasaidia walengwa kuwa katika makundi ili waweze kujifunza masuala ya kuweka akiba na kuwekeza" amesema
Nae Mnufaika wa TASAF Tatu Ramadhani amesema kuwa yupo katika maonesho hayo kwa ajili ya kuonesha bidhaa ambazo anatengeza baada ya kupata elimu ikiwemo vikapu vya wakinamama, mikanda, bangili kwa kutumia shanga, sabuni pamoja na kava za usukani wa gari.
Amesema kuwa TASAF wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha biashara zao ikiwemo kuwaongezea fedha za mtaji.
No comments:
Post a Comment