NAIBU Katibu Mkuu Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg , Riziki Kingwande amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao na kuwalinda walinzi kwani maadili yameporomoka hivyo amewasihii kundokana na desturi ya kuamini watu kwa urahisi kwani Dunia imeharibika .
Kingwande ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Soya na Kimaha Wilayani Chemba ambako viongozi wa juu wa UWT unafanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo.
Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.Mary Chatanda Novemba 23,2023 umeendelea na ziara yake ikiwa ni siku ya pili umefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani humo.
"Wazazi naombeni tuwajibike katika kuwalea watoto wetu kwenye msingi mzuri kwani ndio viongozi wa leo na kesho yao ambayo bado wanayo kubwa ,hatuwezi kukaa kimya hii hali ya sasa hivi ambayo watoto wetu wanaharibiwa kwa kukatishwa ndoto zao na miili yao utasikia huko mara mtoto amelaitiwa mara kabakwa hizi tabia tuzikomeshe " Amesisitiza Ndg. Kingwande
Vilevile, Ndg .Kingwande amefanikiwa kusikiliza kero za wananchi hao na kuzipatia ikiwemo ahadi ya muda mrefu ya gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati ya Soya na zingine ameielekeza Halmashauri ya Chemba kuwafanikishia wananchi wake likiwemo suala la TASSAF ,Barabara, ujenzi wa shule Vyumba vya madarasa 4 katika Shule ya Chang'ombe na Kata hio,pamoja mengine ambayo yatapatiwa ufumbuzi .
Kingwande amefanikiwa kutembelea mradi wa Ujenzi wa Vyumba 4 vya madarasa na Ofisi 3 katika Shule ya Msingi Mwaikisabe wenye thamani ya Shilingi 90,000,000 (Millioni tisini) kituo cha Afya zahanati ya Soya iliyopo kata ya Soya pamoja na kusikiliza kero za wananchi .
No comments:
Post a Comment