Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mzava (aliyesimama) akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwadila wilayani Maswa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwadila wilaya ya Maswa.
Wakazi wa Kijiji cha Mwadila wilaya ya Maswa wakionesha Ramani ya mpango wa Ardhi katika Kijiji hicho kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwadila wilaya ya Maswa.
Wakazi wa Kijiji cha Mwadila wilaya ya Maswa wakionesha Ramani ya mpango wa Ardhi katika Kijiji hicho kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii.
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Mwadila wilaya ya Maswa waliohudhuria Mkutano wa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii.
Mjumbe ajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Asia Halamga (kulia) akikabidhi hati milki ya Ardhi kwa mwananchi wa Kijiji Cha Mwadila wilayani Maswa.****************
Na Hassan Mabuye, SimiyuKamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji
Usalama wa Milki za Ardhi katika vijiji vya Mwadila, Zabazaba na Igongwa katika
halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Akieleza mbele ya wakazi wa
vijiji hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii, Mhe. Timotheo Mzava wakati wa Ziara ya kamati hiyo wilayani humo
amesema ni jambo la kuipongeza Wizara ya Ardhi katika kuwezesha mradi huo
kuweka mazigira mazuri ya matumizi bora ya ardhi.
Amesema kuwa kulingana na
maelezo waliyoyapata kutoka kwa watekelezaji wa mradi huo pamoja na wananchi wa
vijiji hivyo sambamba na kuonyesha ramani zilizotengwa kwa ajili ya kuonyesha
matumizi bora ya ardhi kwa pamoja wamejiridhisha kuwa kazi imefanyika vizuri.
“Kazi yetu sisi kamati hii ya bunge ambayo
imetufikisha wilayani Maswa ni kufuatilia na kujiridhisha fedha zilizotolewa na
bunge zaidi ya Tsh. Bilioni 3 kwa ajili
ya kutekeleza mradi huu katika wilaya hii zimefika na kufanya kazi iliyokusudiwa
kwa ufanisi.
“Maelezo tuliyopewa na
watendaji wa serikali wanaotekeleza mradi huu na yale mliyoyatoa ninyi wananchi
na mawasilisho kwetu kupitia ramani tumejirisha
sisi kama kamati kuwa kazi imefanyika vizuri.”amesema.
Amesema kwa kuwa mradi huo unatekelezwa na serikali kwa kupitia wizara
ya ardhi na wananchi wameshirikishwa ni mradi mzuri ambao unafaida nyingi
zikiwemo kuondoa tatizo la migogoro ya mipaka katika ya Kijiji na Kijiji,
mipaka ya mashamba sambamba na kuongeza thamani ya Ardhi.
‘Katika mipango yenu mliyoweka
kama kijiji mkakubaliana kutenga maeneo mathalani eneo litumike kama eneo la
akiba, eneo la kilimo, eneo la kuchungia ni vizuri likatumika kama
ilivyokusudiwa na si vinginevyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amesema kuwa wilaya hiyo inakwenda kupima vijiji
vyote 120 kwa mchanganuo kuwa vijiji 106 vitapimwa, Vijiji 5 vitaingizwa katika
mji wa Maswa na vijiji 9 vitapewa hadhi ya kuwa miji midogo na wananchi
watapatiwa Hati Milki za Ardhi.
“Tunapopima ardhi hivi
tunaondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa
mingi katika jamii na hii ndiyo dawa yake na hapa Maswa tumeweza kutenga Hekta
77,000 kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji, Hekta 481 kwa ajili ya taasisi za
serikali na Hekta 713 kwa ajili ya kuweka Viwanda na Uwekezaji,”amesema.
Naye Mkuu wa wilaya ya Maswa,
Aswege Kaminyoge ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuona
ipo sababu ya kuleta mradi huu katika Wilaya hiyo kwani ni mradi wenye tija kwa
wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa.
“Mradi huu utakuza uwekezaji
katika sekta ya ardhi hapa wilayani Maswa na kuhakikisha ushirikishwaji wa
wananchi katika usimamizi wa ardhi yao kwa maendeleo endelevu,”amesema.
HABARI PICHA
1.
2.
3.
4.
5.
No comments:
Post a Comment