Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Taasisi, Mashirika na Wabunge leo Oktoba 26, 2023 wametembelea banda la Tume ya Madini kwenye maonesho yanayoendelea katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupata maelezo kuhusu majukumu ya Tume sambamba na fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini wameomba elimu kuhusu shughuli za upimaji wa madini zinazofanywa na maabara ya Tume kuendelea kutolewa kwa wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na ubora wake wa kimataifa na kuhakikisha wadau wengi zaidi wa madini wananufaika na uwepo wa maabara hiyo.
No comments:
Post a Comment