Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limewataka waandishi wa habari kuripoti maramoja wanapopata madhila wakati wanatimiza majukumu yao ili waliowafanyia hayo waweze kuchukuliwa hatua.
Hayo yamesemwa Oktoba 26, 2023 na Mkuu wa Polisi Jamii mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Gallus Hyera wakati wa mdaharo wa majadiliano kati ya Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe na Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kuhusu madhila wanayopata waandishi wa habari wakati wanatekeleza majukumu yao.
ACP Hyera amesema Jeshi la Polisi linasisitizia askari wake kuwa na nidhamu, kufanya kazi kwa weledi na haki lakini hapa na pale askari mmoja mmoja anakengeuka na kufanya kinyume na maelekezo hayo.
"Akikosea askari mmoja isihesabike kuwa askari wote ndivyo walivyo bali nyie wanahabari mkipata tatizo lolote kuhusu askari toeni taarifa kwa viongozi wao Ili hatua zichukuliwe mapema" amesema ACP Hyera.
No comments:
Post a Comment