Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Onesho la Kimataifa la Swahili International Tourism Expo (S!TE) katika ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Thereza Mugobi.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Onesho la
Kimataifa la Swahili International Tourism Expo (S!TE) katika ukumbi wa
Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)(hayupo
pichani) katika kikao kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Dunstan Kitandula (Mb)(wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB), Damas Mfugale (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,
Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Thereza Mugobi mara baada ya kikao na waandishi wa habari kuhusu Onesho la
Kimataifa la Swahili International Tourism Expo (S!TE) katika ukumbi wa Mikutano
wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.***********
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa maandalizi ya Onesho la saba la Utalii la
Kimataifa la Swahili International Tourism Expo – S!TE 2023 yamekamilika
ambapo kwa mara ya kwanza kutakuwa na
bustani ya wanyama hai
Akizungumza kwenye Mkutano na
Waandishi wa Habari leo Oktoba 3, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani
City, Jijini Dar es Salaam amesema onesho hilo litafanyika kuanzia Oktoba 6 - 8
mwaka huu ambapo wageni na wadau muhimu wa sekta kutoka maeneo mbalimbali
duniani watahudhuria.
“Katika kipindi chote onesho
hili limekuwa jukwaa muhimu na lenye ushawishi kwa wadau mbalimbali ndani na
nje ya nchi walio katika mnyororo wa huduma za utalii.” Amefafanua Mhe. Kairuki
Waziri Kairuki amewataja
baadhi ya wadau watakaoshiriki kwenye maonesho ya mwaka huu kuwa ni pamoja na
Mabalozi wa nchi mbalimbali, Bodi za Utalii kutoka nchi za Afrika zikiwemo
Uganda na Malawi, Waoneshaji (Exhibitors) zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya
nchi. Wanunuzi wa biashara za utalii (Buyers) zaidi ya 70 kutoka katika masoko
yetu ya Kimkakati ya kimataifa hususan, Ulaya, Amerika na Asia.
Aidha, amesema onesho la mwaka
huu litapambwa na Bustani ya Wanyamapori hai ili kuwavutia watembeleaji (visitors)
na kuhamasisha Utalii wa ndani, pamoja na Jukwaa la Uwekezaji la Utalii
(Tanzania Tourism Investment Forum-TTIF) na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza
kuja kutembelea na kuona hazina na urithi wa utalii wa Tanzania pia
“Natoa rai kwa watanzania,
wawekezaji, na wadau wengine wa utalii kushiriki kikamilifu onesho la SITE
2023, ambalo ni fursa ya muhimu kukutana na wadau wenzenu waliopo katika
mnyororo wa thamani wa Sekta ya Utalii, ili kwa pamoja tuhakikishe sekta hii
inapiga hatua tukitambua melengo makubwa tuliyonayo ya kufikia watalii milioni
5 na mapato ya Dola za Marekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025. Halikadhalika
kuendelea kuitangaza nchi yetu kimataifa kupitia utambulisho wetu wa Tanzania,
Unforgettable na Programu ya Tanzania – The Royal Tour.” Amesisitiza Mhe.
Kairuki.
Waziri Kairuki ametoa
wito kwa
wadau mbalimbali kutembelea mtandao wa site.tanzaniatourism.go.tz ili
kuona mambo muhimu yanayohusu onesho hili ikiwa ni pamoja na semina mbalimbali, midahalo inayoangazia mada
za utalii na fursa za uwekezaji ambapo amesema Kauli mbiu ya Onesho la S!TE
2023 ni: Utalii Unaowajibika kwa Maendeleo Jumuishi.
“Natoa rai kwa watanzania, wawekezaji, na wadau wengine wa utalii kushiriki kikamilifu onesho la SITE 2023, ambalo ni fursa ya muhimu kukutana na wadau wenzenu waliopo katika mnyororo wa thamani wa Sekta ya Utalii, ili kwa pamoja tuhakikishe sekta hii inapiga hatua tukitambua melengo makubwa tuliyonayo ya kufikia watalii milioni 5 na mapato ya Dola za Marekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025. Halikadhalika kuendelea kuitangaza nchi yetu kimataifa kupitia utambulisho wetu wa Tanzania, Unforgettable na Programu ya Tanzania – The Royal Tour.” Amesisitiza Mhe. Kairuki.
No comments:
Post a Comment